Mgombea ubunge katika jimbo la Mafinga Mjini Cosato
Chumi akiomba kura wananchi wa mtaa wa Lumwago
Mgombea ubunge katika jimbo la Mafinga Mjini Cosato
Chumi akiwa kwenye mkutano wa kampeni
Na Fredy Mgunda,Mafinga.
MGOMBEA ubunge katika jimbo la
Mafinga Mjini Cosato Chumi kuendelea kuiomba serikali kuruhusu wananchi kufanya
biashara masaa ishirini na manne Kama ilivyo katika kusafirisha mazao ya misitu.
Akizungumza kwenye mkutano wa wa
kuomba kura kwa wananchi wa mtaa wa Lumwago,Chumi alisema kuwa ilikukuza uchumi
kwa wananchi wa jimbo la Mafinga Mjini wanatakiwa kufanya shughuli za
kimaendeleo kwa masaa yote ishirini na nne.
Chumi ambaye anayetetea nafasi yake,
amesema kama ambavyo Serikali ilikubali kuruhusu malori kusafiri masaa ishirini
na manne anaamini Serikali itaridhia wananchi wa Mafinga wafanye biashara masaa
24.
“Huu ni Mji wa kibiashara, sio Saa
nne tu polisi hawa hapa wanataka ufunge biashara, haiwezekani, nitaongoza hoja
ya kubadilisha sheria Watu wajiachie wafanye biashara usiku na mchana”alisema Chumi
Alisema Wananchi wa Mafinga wana
bidii ya kufanya kazi, kufanya biashara masaa ishirini na manne itaongeza
kipato cha mtu mmoja mmoja, Halmashauri na Taifa kwa ujumla.
Aidha Chumi alisema wafanyabiashara
wanatakiwa kufanyabiashara muda wowote ili kuongeza kipato chao kama ilivyokuwa
kwenye nchi zilizondelea hasa kwenye miji midogo inayokuwa kiuchumi
Post A Comment: