Na Woinde Shizza, Arusha

Mgombea ubunge wa Jimbo la Karatu kupitia chama Cha mapinduzi Daniel Awack amewahaidi wananchi wa Jimbo  hilo waliopo katika kata ya Mang'ola kuwajengea shule ya bweni ya wasichana Ili kupunguza tatizo la mimba  kwa wasichana wa Jimbo Hilo

Aliyasema hayo Jana wakati wa uzinduzi wa kampeni za jimbo ilo  ulioufanyika katika kiwanja Cha Mang'ola barazani  uliopo katika kata hiyo ambapo alifafanua kuwa wanafunzi wengi wamekuwa wakishindwa kuendelea na masomo kutokana na kupata mimba kipindi wakiwa shuleni

"Kumekuwa na tatizo la mabinti wetu kupata mimba wakiwa shuleni na hii inatokana na vishawishi wanavyovipata uko njiani wakati wakielekea shuleni sasa nawahaidi mkinipa Kura zenu nitahakikisha najenga shule ya wasichana ya bweni ambayo itasaidia kupunguza tatizo hili kwani wanafunzi watakuwa wanakaa shuleni namaanisha katika mabweni  hivyo itasaidia kuepuka vishawishi ambavyo wanapata wakiwa njiani "alibainisha Awack

Aidha pia aliwahaidi wananchi wa Jimbo Hilo kuwaekea wakili ambaye atakuwa anawasaidia katika kesi zao ili wasiweze kuzulumiwa katika kesi zao mbalimbali,ambapo pia alibainisha katika Jimbo la Karatu kumekuwa na changamoto ya barabara kwa kipindi Cha muda mrefu nakuwaaidi kuwa iwapo watampa nafasi ya kuwawakilisha bungeni atahakikisha barabara hiyo inajengwa katika kiwango Cha lami


"Najua hapa Mang'ola wananchi wengi wanategemea kilimo Cha umwagiliaji  na tatizo lao kubwa Ni uhaba wa visima pamoja na miundo mbinu ya umwagiliaji nathani mnanijua Mimi mwenyewe ni mkulima mkininipa kura matatizo yote haya nawahaidi nitayamaliza na labda niwaambie wakulima wadogo kutasaidia pia wakulima wadogo kuwatafutia watu watakao wapa mitaji ya kukuza kilimo Chao"alifafanua Awack

Akiongea wakati wa kumnadi mgombea ubunge huyo pamoja na kumuombea Rais Kura  mwenyekiti wa CCM mkoa wa Arusha Zelothe Steven Zelothe alisema kuwa wamchague Dr magufuli kwakuwa Ni miadilifu ,mtetezi wa wanyonge,mchapakazi,mwanamapinduzi wa kweli,Ni kiongozi mpenda haki,anachukia rushwa ,anachukia ufisadi na pia ni mtetezi wa yale anayoyaamini hivyo wasiache kumchagua na katika kipindi chake Cha miaka mitano ametekeleza ahadi zake zote kwa vitendo.


Naye mgombea udiwani wa kata ya Qurus   Danstan Panga aliwataka wananchi wa Karatu kumchagua mbunge huyo kwa kuwa Kwanza Ni mkazi wa Jimbo lao pia ni mtoto wa mkulima hivyo ataweza kupeleka matatizo yao bungeni ili yaweze kutatuliwa .

"ndugu Wana Karatu tumeongozwa na upinzami miaka 25 hapa lakini hakuna Maendeleo yoyote tulioletewa  barabara Ni mbovu ,huduma za afya atupati vyema ,shule za bweni kwa watoto wetu wakike niseme tu 25 imetosha tunaitaji mabadiliko ninaomba tusifanye makosa ya nyuma"alisema Panga

Akimuombea Kura mgombea Urais kwa tiketi ya chama Cha mapinduzi ambaye pia Ni mwenyekiti wa CCM  taifa pamoja na mgombea Ubunge Jimbo la Karatu ,Balozi Batilda Burian aliwataka wananchi kuwapa Kura za kishindo wagombea hawa ili wakaweze kuwaletea Maendeleo  na kuwasisitiza wafuate kauli mbio yao inayosema miaka 25 ya kuongozwa na ushindani inatosha

Share To:

msumbanews

Post A Comment: