Msaidizi wa Mufti Shehe Yusuph Hassani Tonge akizungumza na waandishi wa habari kuishukuru Taasisi ya Uturuki akiwemo Rais wao kwa msaada huo
Watu wakiendelea na uchinjaji wa ngombe
uchinjaji wa ngombe ukiendelea
Wachinjaji wakiendelea kuchuna ngombe kama wanavyoonekana
Mbuzi nao wakichunwa kwa ajili ya sikukuu
Baadhi ya viongozi wa Taasisi za Kiislamu wakipatia ngombe ambao walitolewa kwao kwa ajili ya sikuuu ya Eid El Fitri
WATANZANIA
wametakiwa kuendelea kuitunza amani iliyopo hapa nchini hasa wakati nchi
ikielekea kwenye uchaguzi mkuu ambao utafanyika Octoba 28 mwaka huu uweze
kufanyika kwa amani na salama
Wito
huo ulitolewa na Msaidizi wa Mufti Shehe Yusuph Hassani Tonge Julai 31 mwaka
huu wakati wa sikukuu ya Eid El Fitri mara baada ya kumalizika kwa zoezi la uchinjaji
wa wanyama mbalimbali ikiwemo ngombe, mbuzi na kondoo.
Ikiwa
ni zawadi kutoka kwa watu wa uturuki kwa ajili ya waislamu kupata sadaka ya
kwendaa kusheherekea sikukuu hiyo ambayo ni maalumu kwa ajili ya uchinjaji.
“Tumekuja
Tanga kuchukua wanyama ambao wametolewa na wafadhili mbalimbali kutoka nchini
Uturuku wakiwemo wasilamu pamoja na Rais wao Recep Tayyıp Erdoğa hivyo tunashukuru sana kwa msaada
huu na tunaomba mwenyezi mungu akijalia watuletee tena mwaka ujao”Alisema
Msaidizi wa Mufti.
Shehe
Tonge ambaye pia ni Mjumbe wa Halmashauri Kuu Taifa ya Waislamu nchini alisema
waislamu hutumia siku hiyo ya kuchinja kwa sababu ya kumbukumbu ya nabii
Ibrahimu alipopewa amri ya kumchinja mwanaye na badae kuletewe kondoo.
Alisema
hiyo ni ishara ya amani na kwa sababu watanzania wanaelekea kwenye uchaguzi mkuu
tukio hilo la kutoa sadaka kwa mwenyezi mungu liisaidie nchi yetu kuingia
kwenye uchaguzi mkuu wa amani na umalizike salama.
Post A Comment: