Wanaume kijiji cha Engalaoni kata ya Mwandeti wamejitokeza kwa wingi kwenye kilele cha Maadhimisho ya Wiki ya Unyonyeshaji Duniani na kukiri kupata uelewa mkubwa juu ya umuhimu wa mama kumnyonyesha mtoto miezi 6 ya mwanzo bila kumpa chakula kingine chochote.
   Mafunzo ya unyonyeshaji yaliyotolewa kwenye sherehe za Kilele cha Maadhimisho hayo, yaliyofanyika kwenye Kijiji cha Engaloni, yamevuta hisia za wananume hao, kwa kushangazwa na kuchelwa kufahamu, umuhimu wa kunyonyesha mtoto kwa miezi sita ya mwanzo bila kumpatia mtoto chakula kingine wala maji ya kunywa.
    Wamesema kuwa, wamekuwa wakisikia kina mama wakisemasema hayo, lakini hawakuamini kama inawezekana, mtoto kuishi miezi sita bila kunywa hata maji, jambo ambalo wamekiri kuwafungua ufahamu na kukubali mabadiliko hayo kufanyika kwenye familia zao.
   "Tumekuwa tukisikia kina mama wakisema wanantakiwa kunyonyesha mtoto miezi sita bila kumpa hata maji ya kunywa lakini tulidhani ni kitu ambacho hakiwezekani kwa binadamu kuishi bila kunywa hata maji miezi sita, kwa elimu hii, imetuondoa gizani, tumepata ufahamu mkubwa, tutaanza kuufanyia kazi kwenye familia zetu" . Wamesema wanaume hao wa Engalaoni
      Aidha wamekiri kufahamamu pia, faida za kumnyonyesha mtoto miezi sita ya mwanzo bila kumpa chakula kingine ikiwa ni pamoja na kuimarisha kinga ya mwili itakayo mkinga mtoto dhidi ya kushambuliwa na maradhi, kuimarisha akili ya mtoto pamoja na mwili wa mtoto kuimarika kimakuzi.
     Lakini pia wanaume hao, wamesikitishwa na madhara makubwa  yanayoweza kumpata mtoto asiponyonyeshwa kwa utaratibu, na kupata madhara makubwa katika maisha yake,  ikiwemo kuharibu mfumo wa mmeng'enyo wa chakula kwa mtoto, udumavu wa mwili na akili kwa mtoto, jambo ambalo wamethibitisha linaweza kuepukika kupitia elimu ya unyonyeshaji waliyoyapata.
   Hata hivyo wanaume hao, wamesema kuwa wako tayari kubadilika na kushirikiana na mwanamke katika kipindi chote cha ujauzito, kujifungua na kipindi cha siku 1000 za kunyonyesha, sambamba na kumuwezesha mama kupata lishe bora ili mtoto apate maziwa yenye virutubisho vya kutosha kwa afya ya mtoto na jamii wa maendeleo ya Taifa.
    Kilele cha Maadhimisho ya Wiki ya Unyonyeshaji Duniani 2020, yamefanyika kwenye kijiji cha Engalaoni kata ya Mwandeti na Kijiji cha Lemanyata kata ya Olkokola, halmashauri ya Arusha huku jumla ya vijiji 14 vkiwa vimepata mafunzo rasmi ya unyonyeshaji katika wiki nzima ya maadhimisho ua unyonyeshaji Duniani.

PICHA ZA MATUKIO KIJIJI CA ENGALAONI















Share To:

Post A Comment: