Umoja wa Vijana wa Chama Chama Mapinduzi Mkoa wa Ruvuma kupitia Mwenyekiti wake Raymund Mhenga leo amepongeza Chama cha Mapinduzi Taifa chini ya Mwenyekiti wake Dr John Pombe Magufuli kwa kufanya uteuzi bora wa Wagombea wa nafasi za Ubunge na  Uwakilishi.

Akizungumza na Waandishi wa Habari leo Mwenyekiti Mhenga amesema Vijana wa Mkoa wa Ruvuma na Wilaya zake zote wamepokea kwa mikono miwili uteuzi wa Wabunge watakaopeperusha bendera ya CCM kwenye Uchaguzi huu,sambamba na wabunge wa Viti Maalumu.Mwenyekiti alitanabaisha kuwa wao wamepokea kwa furaha uteuzi huo ambao umewarudisha watu sahii na wanaokubalika na jamii na hivyo kama vijana wao kazi yao ni kuwaunga mkono na kuongoza jeshi la kutafuta kura kwa Madiwani,Wabunge wateule hao na Baba yetu Rais Dr Jonn Pombe Magufuli na wataifanya kazi hiyo kwa moyo wote pasipo kuchoka mpaka ushindi wa Asilimia 99% upatikane.

Imetolewa na Katibu Hamasa na Chipukizi
Ndugu Twaha Saanane Mchata
Uvccm Mkoa wa Ruvuma
Share To:

msumbanews

Post A Comment: