MGOMBEA
Ubunge Jimbo la Tanga (CCM) Ummy Mwalimu kulia akichukua fomu ya kuomba
kuwania nafasi hiyo kutoka kwa Msimamizi wa Uchaguzi wa Jimbo la Tanga
Daudi Mayeji leo |
MGOMBEA Ubunge Jimbo la Tanga (CCM) Ummy Mwalimu akiwaonyesha fomu za kuwania Ubunge Jimbo la Tanga mara baada ya kukabidhiwa na Msimamizi wa Uchaguzi Jimbo la Tanga leo |
Umati
Mkubwa wa wana CCM waliojitokeza kumsindikiza Waziri Ummy wakati
alipofika ofisi za CCM wilaya ya Tanga eneo la Masiwani Jijini Tanga
Waziri Ummy kushoto akiwa na Wabunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Tanga CCM
wakati alipokwenda ofisi za CCM wilaya ya Tanga kudhaminiwa na chama
chake
KATIBU wa CCM wilaya ya Tanga Salum Kidima akizungumza
MWENYEKITI wa CCM wilaya ya Tanga Meja Mstaafu Mkoba akizungumza
MGOMBEA Ubunge wa Jimbo la Tanga na Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii
Jinsia Wazee na Watoto Ummy Mwalimu akiwa na wananchi na wana CCM wakati
alipofika ofisi za CCM wilaya ya Tanga kudhaminiwa
MGOMBEA
Ubunge Jimbo la Tanga (CCM) Ummy Mwalimu leo amelitikisa Jiji La
Tangawakati alipokwenda kuchukua fomu ya kuwania Ubunge wa Jimbo hilo
huku
akiwa anasindikizwa na umati mkubwa wa wananchi na wanachama wa chama
hicho.
Ummy
ambaye pia ni Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto msafara
wake ambao ulikuwa ukisindikizwa na magari, pikipiki huku wananchi wengine
wakiwa pembezoni mwa barabara wakimshangilia na kumpungia mikono.
Msafara
huo ulizunguka maeneo mbalimbali kwenye Jiji hilo na baadae kufika kwenye ofisi
za Msimamizi wa Uchaguzi Jimbo la Tanga kwa ajili ya kuchukua fomu za kuwania
kiti hicho.
Akizungumza
mara baada ya kuchukua fomu Ummy alisema kwamba anawashukuru halmashauri kuu ya
CCM kwa kumwamini na kumpitisha kuwania Ubunge Jimbo la Tanga huku akiahaidi
kufanya kampeni za kiistarabu shuka kwa shuka ,kitanda kwa kitanda na uvungu
kwa uvungu
Alisema
kwa anawashukuru wajumbe wa mkutano mkuu wa CCM wilaya ya Tanga ambao
walimpitisha kwa kura za kishindo kwa kumpendekeza kuwa mgombea wa Ubunge Tanga
mjini .
“Wajumbe
wamekuwa ni watu maarufu sana lakini wajumbe wa mkutanbo mkuu wa Tanga
mjiniwaoi kwangu mimi wamenitendea haki kwangu
mm wamenipa heshima niwashukuru sana
wenyeviti wa ccm kutoka matawi yote 153 ya jiji la Tanga, makatibu tawi wote,
na makatibu wenezi wote pamoja na wajumbe waliotoka kwenye ngazi ya matawi,’’alisistiza
Ummy Mwalimu.
Nilipata
heshima ya kuwa Mbunge viti maalumu miaka 10 na mshahara wa mbunge wa viti
maalumu na jimbo ni mshahara mmoja
ningekuwa nimeshamaliza mchezo lakini kwasababu ya shauku na mapenzi
makubwa kwa wanantanga hulka na hamu yangu ya kuipenda Tanga mjini ninataka kuiona
yenye heshima na hadhi yake",amesema.
Aidha
Waziri Ummy alituma salamu kwa wapinzani wake kuhakikisha wanajipanga
vyema kwani wao watafanya kampeni za maendeleo na kampeni za
kistaarabu na heshima kampeni
zinazoakisi hadhi,utu na heshma yab wanatanga kutokana na hulka ya
wanatanga
kuwa wastaarabu.
‘’Nitume
salamu kwa watani zetu walioingia kwenye kinyanganyiro hiki kuwa sisi tutafanya
kampeni za ustaarabu, heshima na maendeleo lakini wakituchokoza …….wataweza
kweli..hata wakiungana..matusi kututukana,’’alibainisha Ummy.
Katika
hatua nyingine Waziri Ummy alisema watahakikisha wanafanya kampeni za kistaarabu
nyumba kwa nyumba, shuka kwa shuka, kitanda kwa kitanda na uvungu kwa uvungu
kuhakikisha jimbo linarudi katika chama cha mapinduzi CCM.
Post A Comment: