Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Utafiti wa Kilimo nchini (TARI), Dk Geofrey Mkamilo akisisitiza jambo wakati akieleza hatua kadhaa zilizofikiwa na taasisi hiyo mpaka sasa, kwenye Maonesho ya Nanenane Kitaifa mwaka huu, yanayofanyika eneo la Nyakabindi, Bariadi mkoani Simiyu.
Baadhi ya wataalamu wa Taasisi ya Utafiti wa Kilimo nchini TARI wakifurahia moja ya kazi za usindikaji zinazofanywa na TARI kwa kunyanyua juu chupa yenye mvinyo uliotengenezwa kwa 'Bibo la Korosho' , kwenye maonesho ya nanenane kitaifa mwaka huu, yanayofanyika eneo la Nyakabindi, Bariadi mkoani Simiyu.

Mkurugenzi wa TARI Utawala na Menejimenti ya Rasilimali Watu, Nigel Msangi akizungumza kwenye banda la Taasisi hiyo.
Mtafiti wa zao la Miwa TARI, Diana Nyanda (kushoto) akimkabidhi Tatu Mzee juice ya miwa iliyotengenezwa na taasisi hiyo.
Mtafiti wa TARI, Kassim Masibuka akitoa huduma kwa wakulima waliohudhuria kwenye banda la taasisi hiyo.
Huduma kwa wakulima kwenye banda hilo zikiendelea kutolewa.
Mkurugenzi wa TARI Ilonga, Dk Joel Meliyo akishiriki kutoa huduma kwenye banda la Taasisi hiyo.
Mkurugenzi TARI Mlingano Dk Catherine Senkoro akitoa mafunzo ya zao la Katani kwa wakulima na wadau wa kilimo kwenye banda la Wizara ya Kilimo Nyakabindi mkoani hapa jana.
Mratibu zao la Korosho Kituo cha Utafiti wa Kilimo TARI Naliendele, Dk. Geradina Mzena (kulia) akizungumzia na baadhi ya wateja waliotembelea banda hilo.


Mtaalamu wa Maabara TARI Michael Madumba akishiriki kutoa huduma.
Baadhi ya wataalamu wa Kituo cha Utafiti wa Kilimo nchini TARI wakifurahia moja ya kazi za usindikaji zinazofanywa na TARI.
Msimamizi wa Idara ya Uhaulishaji Teknolojia na Mahusiano, Dk Richard Kasuga akizungumza.
Mwonekano wa shamba darasa zao la Mtama kwenye kituo cha TARI Nyakabindi.


Mwonekano wa shamba darasa  la mbogamboga kwenye kituo cha TARI Nyakabindi.

Mwonekano wa shamba darasa zao la Mahindi kwenye kituo cha TARI Nyakabindi.
Mwonekano wa shamba darasa zao la ndizi kwenye kituo cha TARI Nyakabindi.
Mwonekano wa shamba darasa zao la Katani kwenye kituo cha TARI Nyakabindi.


Na Godwin Myovela, Simiyu



MOJA ya vivutio vya aina yake kwenye maonesho ya Nanenane Kitaifa mwaka huu ni namna Taasisi ya Utafiti wa Kilimo nchini (TARI) ilivyokuja na shehena ya teknolojia zake ambazo ni dhahiri zinaakisi kauli mbiu yao yaani ‘Kuleta Mapinduzi ya Kilimo’ huku umahiri mkubwa ukiwekezwa kwenye eneo la mashamba darasa kwa lengo la kuhaulisha teknolojia kwa mkulima ambazo ni matokeo ya utafiti.

Baadhi ya wakulima waliohudhuria maonesho hayo eneo la Nyakabindi, mkoani Simiyu jana, walisema wameshangaa kuona namna TARI ilivyofanikiwa kuleta teknolojia zilizopelekea kustawisha kwa tija vipando vya mazao tofauti takribani 30 yenye aina mbalimbali za mbegu.

“Ukitazama afya iliyopo kwenye shamba darasa hili mpaka unapata mwamko, mazao yamestawi vizuri sana, nimekuja kupata maarifa kwa wataalamu wa Tari waliopo hapa ili nianze safari yangu mpya kuelekea kwenye mapinduzi ya kilimo,” alisema mkulima Alexander Bukulu.

Akizungumza kwenye viwanja vya maonesho hayo, Mkurugenzi Mkuu wa TARI, Dk Godfrey Mkamilo alisema pamoja na mambo mengine, jukumu kubwa la taasisi hiyo nikuhakikisha matokeo ya utafiti wake yanasambazwa kwa wakulima wote tena kwa wakati.

“Lengo letu ni kuongeza uzalishaji tija ili kilimo kiweze kuchangia kwenye uchumi wa mkulima mmoja, familia na taifa kwa ujumla. Na tayari kupitia kanda zote saba za kilimo zilizopo tumeanzisha mashamba mahiri kwa ajili ya usambazaji wa teknolojia zetu kwa wakulima.

Mkamilo aliyataja baadhi ya mashamba endelevu yatakayoendelea kuhudumia wakulima kwa mwaka mzima kwa azma chanya ya uhaulishaji wa teknolojia kuwa ni pamoja na shamba la Nyakabindi, lililopo Bariadi mkoani hapa, Nyamhongoro mkoani Mwanza, John Mwakangale mkoani Mbeya na JK. Nyerere Morogoro.

“Baada ya kumalizika kwa Nanenane hii tutaanza kutoa mafunzo kwenye Halmashauri kupitia maafisa ugani na wakulima wao, shabaha yetu kama TARI teknolojia hizi ziwafikie wakulima walio wengi ili kuleta mapinduzi ya kilimo,” alisema Mkamilo.

Kwa upande wake, Msimamizi wa Idara ya Uhaulishaji Teknolojia na Mahusiano, Dk. Richard Kasuga alisema taasisi hiyo iliyoanzishwa kwa sheria ya Bunge namba 10, 2016 jukumu lake kubwa ni kutafiti, kuhamasisha, kusimamia na kuratibu utafiti wa kilimo nchini.

“Hapa Nyakabindi kwenye kituo chetu hiki tumepanda mazao yote jamii ya nafaka kama mahindi, mtama, uwele, ulezi na mpunga, pia tuna jamii ya mikunde kama choroko, kunde, maharage yenye virutubisho vya vitamini A na zink…ambayo ni muhimu katika makuzi ya binadamu, na mazao mengine mengi” alisema Kasuga

Alisema lengo la kuweka kituo hicho cha teknolojia ni kumwezesha mkulima kujifunza kuanzia hatua ya kwanza ya uandaaji wa shamba kwa vitendo, afya ya udongo na ubora wa mbegu kulingana na jiografia za mahali husika.

“Mkulima unapotaka kulima zao lolote unashauriwa njoo uwaone wataalamu kwa ushauri ili hatimaye kuweza kuzalisha kwa tija na kibiashara,” alisema Kasuga.
Share To:

Post A Comment: