Ili kudhibiti ubadhirifu wa fedha za Umma zinazotolewa kufanya miradi ya Maendeleo maeneo mbambali ya mkoa wa Manyara,Taasisi ya kuzuia na Kupambana na rushwa (TAKUKURU) Mkoa wa hapo, imeanza kutembelea na kukagua miradi inayoendelea kwa sasa mkoani humo.
Afisa wa TAKUKURU wilayani Kiteto kitengo cha udhibiti na ufuatiliaji wa miradi ya Maendeleo Emmanuel Manyutwa, amefika katika shule ya Msingi Partimbo kukagua maendeleo ya ujenzi wa choo chenye matundu (20) kujiridhisha na fedha iliyotumika ukilinganisha na kazi iliyofanyika.
Hata hivyo baada ya kufanya ukaguzi, Manyutwa ameonekana kuridhika na maendeleo ya mradi.
Kwa mujibu wa Mkuu wa TAKUKURU Mkoa wa Manyara Holle Makungu, Mradi huo ni kati ya miradi inayotekelezwa wilayani kiteto kupitia mpango wa SWASH (School Water,Sanitation and Hygen) ambao Thamani yake ni shilingi Milioni 21,756,000/ hadi kukamilika.
Post A Comment: