Mratibu wa Mradi wa Maendeleo Kwamsisi wa Shirika la World Vision Tanzania Jackline Kaihura kushoto akishiriki kucheza ngoma wakati wa kilele cha wiki ya unyonyeshaji iliyofanyika kata ya Komkonga wilayani Handeni mkoani Tanga.

Mratibu wa Mradi wa Maendeleo Kwamsisi wa Shirika la World Vision Tanzania Jackline Kaihura kushoto akiwa na Mkuu wa wilaya ya Handeni Toba Nguvila
Wananchi kutoka maeneo mbalimbali Kata ya Komkonga wilayani Handeni wakiwa kwenye foleni kwa ajili ya uandikishaji wa vyeti vya watoto wao wakati wa kilele cha wiki ya unyonyeshaji iliyofanyika kata ya Komkonga wilayani Handeni mkoani Tanga.
 

SHIRIKA la World Vision Tanzania limesema kwamba suala la unyonyeshaji ni muhimu kwa maendeleo ya mtoto kiafya na kiakili ili aweze kufanya vizuri katika masomo  yake ikiwemo ukuaji mzuri

Hayo yasema na Mratibu wa Mradi wa Maendeleo Kwamsisi wa Shirika la World Vision Tanzania Jackline Kaihura wakati wa kilele cha wiki ya unyonyeshaji iliyofanyika kata ya Komkonga wilayani Handeni mkoani Tanga.

Alisema wao wameamua kushiriki kwenye wiki ya unyonyeshaji kwa sababu shirika hilo ni moja wapo ya shirika ambalo linaangalia ustawi wa mtoto na ustawi wake unaohusisha zaidi afya yake, lishe,elimu na mambo mengine muhimu.

“Labda niseme kwamba suala la unyonyeshaji ndugu zangu ni muhimu sana kwa maendeleo ya watoto kiafya na kiakili kwani inamuwezesha kufanya vizuri katika masomo yake na kupata ukuaji ulio mzuri”Alisema Mratibu huyo.

“Nipende kuihamasisha jamii wanawake, wanaume,vijana na wazee kushiriki kwa pamoja kuhaklikisha mama anapata muda wa kutosha kunyonyesha mtoto aweze kuwa na afya bora na kupata ustawi unaostahiki”Alisema

Hata hivyo alisema kwamba wanafurahishwa kusikia kwenye mkoa wa Tanga Halmashauri ya wilaya ya Handeni imekuwa namba mbili kwenye suala la lishe na unyonyoeshaji kwa sababu shirika hilo limekuwa wilayani humo miaka mingi.

Mratibu huyo alisema kwa hiyo wanayaona matunda yake huku wakihaidi kuendelea kutoa elimu ili kuhakikisha watoto wa mkoa wa Tanga na Tanzania wanapata afya bora na kukua kwenye ustawi mzuri.

Share To:

TANGA RAHA BLOG

Post A Comment: