Wagombea Ubunge wa Chama cha Mapinduzi Jimbo la Kisesa, Luhaga Mpina (kulia) na Leah Komanya Jimbo la Meatu (kushoto ) wakijaza fomu za Tume ya Uchaguzi kuomba kuteuluwa kugombea majimbo hayo kwa ajili ya uchaguzi mkuu mwaka huu.
Mgombea Ubunge Jimbo la Kisesa, Luhaga Mpina akizungumza na madiwani walioteuliwa na CCM kiugombea kwenye kata za Jimbo la Kisesa muda mfupi baada ya kujeresha fomu ya kugombea ubunge 2020.

Mgombea ubunge Jimbo la Kisesa, Luhaga Mpina akifurahia jambo na Mgombea ubunge Jimbo la Meatu, Leah Komanya wakati wakiingia kuchukua fomu ya kuomba kuteuliwa na Tume ya uchaguzi. wengine ni Katibu wa CCM Meatu, Charles Mazuri na Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Meatu, Juma Mwiburi.
Mgombea ubunge Jimbo la Kisesa, Luhaga Mpina akihakiki nyaraka muhimu kabla ya kurejesha fomu ya kuomba kuteuliwa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi kugombea Jimbo la Kisesa. wengine ni Katibu wa CCM Wilaya ya Meatu, Charles Mazuri kulia ni Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Meatu, Juma Mwiburi
Share To:

TANGA RAHA BLOG

Post A Comment: