Na John Walter-Manyara

Flatei Gregory Massay aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Mbulu vijijini  akikabidhiwa fomu ya kugombea ubunge na Msimamizi wa Uchaguzi Jimbo hilo ambaye pia ni  Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya hiyo, Ndg. Hudson Kamoga  leo  Agosti 22, 2020.

Flatei  ambaye alipata fursa tena ya kugombea nafasi hiyo baada ya kupigiwa kura nyingi na wajumbe, amechukua fomu ya kuwania Ubunge Jimbo la Mbulu vijijini  Mkoani Manyara kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) kwa kipindi cha  mwaka 2020-2025.

Umaarufu wa Flatei unakolezwa na kipaji alichonacho cha kuruka  sarakasi ambazo amekuwa akizipiga maeneo mbalimbali ikiwemo wakati wa shughuli za bunge.

Ikumbukwe kwamba, Uchaguzi Mkuu wa kuchagua madiwani,Wabunge na Rais utafanyika   Jumatano tarehe 28 Oktoba 2020.
Kampeni za uchaguzi mkuu zitaanza rasmi tarehe 26 Agosti hadi 27 Oktoba 2020.
Share To:

Post A Comment: