NA MWANDISHI WETU

MDAU wa Maendeleo Wilaya ya Busega ambaye pia ni Kada wa Chama Cha Mapinduzi CCM, Joseph Goryo 'Muddy'  ameeleza kuwa ataendelea kuwa mtiifu na kujijenga zaidi ndani ya Chama maradufu na kueleza kuwa taswira ya ndoto yake bado inaishi.

Goryo ametoa kauli hiyo mapema leo 24, Agosti 2020 mjini hapa na kueleza kuwa, licha ya jina lake kutopenya kwa nafasi ya Udiwani Kata ya Lamadi, anahakika bado ananafasi ya kuitumikia vyema CCM katika maisha yake yote.                 
"Nimejifunza na naendelea kujifunza ukomavu wa kisiasa, Busara kwenye uongozi na kichama.
Matokeo ya Udiwani niliyapokea kwa mikono miwili na kwa sasa tunasaka kura za kishindo kwa Diwani wetu wa Lamadi ambaye jina lake lilibahatika kurudi namuunga mkono kwa asilimia 100" Alieleza Goryo.

Goryo pia amesema atashirikiana na viongozi kumtafutia kura za ushindi mwanzo mwisho.

"CCM chama Dume. Nitaungana na viongozi wa Chama kumuombea kura Diwani wetu. Pia kura za Mbunge na kura za kishindo kwa Rais Magufuli." Alisema Goryo.

Goryo pia alitumia wasaha huo kuwashukuru Wajumbe wote ambao awali walimuezesha kupata kura za ushindi, amewataka kuvunja makundi na  kuwa kitu kimoja kwa mgombea aliyeteuliwa na chama.

Aidha, Goryo ameeleza kuwa, Ndoto yake kuu ni kujenga shule ya ufundi ndani ya Lamdi yenye lengo la kusaidia vijana waliomaliza darasa la Saba na  walioshindwa kujiendeleza elimu ya sekondari.

"Watoto watasoma bure masuala yote ya utayari na ufanisi wa kujiendeleza na kujipa ajira kupitia ufundi na ushonaji watakaopata kwenye shule hii" Alimalizia Goryo.

Goryo ambaye pia ni mkulima na mfugaji wa kisasa, amekuwa mdau mkubwa wa kusaidia jamii ya watu mbalimbali wakiwemo watoto wenye mahitaji maalum ndani ya Busega na mkoa huo wa Simiyu kwa ujumla pia mikoa mingine.

Pia Goryo ni Mjumbe wa Bodi na masuala mbalimbali katika taasisi, shule, jumuiya za kimaendeleo, Balozi wa Haki Elimu, Balozi wa Mtoto wa Kike Edhi salama Wilaya ya Busega.

Mwisho.
Share To:

msumbanews

Post A Comment: