Na John Walter-Manyara
Taasisi ya kuzuia na kupambana na
rushwa wilaya ya Kiteto mkoani Manyara itawarejeshea kiasi cha shilingi milioni 2,050,000
wananchi wakiwemo wachungaji katika
wilaya hiyo, waliotapeliwa na kampuni ya Namaingo Bussiness Agency Ltd
iliyowahaidi kutoa mafunzo ya ujasiriamali na haikufanya hivyo tangu mwaka 2016.
Kaimu mkuu wa Takukuru mkoa wa
Manyara Isdory Kyando amesema awali walipokea malalamiko ya wananchi 41 juu ya
kutapeliwa na mwakilishi wa kampuni hiyo yenye ofisi zake jijini Dar es Salaam,
ambaye aliwawahamasisha wananchi hao wajiunge kwenye vikundi kwa ajili ya
kupatiwa mafunzo ya ujasiriamali ambapo kila mshiriki alitakiwa kutoa kiingilio
cha shilingi 50,000.
Kyando amesema wananchi wote hao
walichangia fedha hizo huku wakisubiri mafunzo hayo bila mafanikio ndipo
walipoamua kufanya mawasiliano na mwakilishi na mkurugenzi wa kampuni hiyo
Bwana Biubwa Ibrahimu bila mafanikio yoyote.
Kaimu mkuu wa Takukuru mkoa wa
Manyara Isdory Kyando ameendelea kusema kuwa baada ya watu hao kuona wanapoteza
haki zao waliamua kufika ofisi za Takukuru wilayani Kiteto kutoa malalamiko yao
dhidi ya Biubwa Ibrahimu ambaye ni mkurugenzi wa Namaingo Business Agency Ltd.
Kyando amesema baada ya kufanya
uchunguzi Bwana Biubwa alikiri kuchukua fedha hizo na kuahidi kuzirejesha na
alitekeleza ahadi hiyo kwa kurejesha fedha zote shilingi milioni 2,050,000.
Post A Comment: