JESHI la kujenga Taifa (JKT) limetangaza nafasi za kujiunga na Jeshi hilo kwa kujitolea kwa vijana wote wa Tanzania Bara na visiwani huku likisisitiza kuwa   halihusiki na kuwatafutia ajira vijana pale wanapomaliza mafunzo hayo.

Akizungumza na waandishi wa habari Mkuu wa tawi la utawala Kanali Julius Kadawi kwa niaba ya  Mkuu wa jeshi la kujenga taifa Meja Jenerali Charles Mbuge amesema utaratibu wa  vijana kuomba kujiunga na kuchaguliwa na mafunzo hayo utaratibiwa na ofisi za Wakuu wa Wilaya na wakuu wa Mikoa  ambapo mwombaji anaishi.

Aidha Kanali Kadawi amesema  maandalizi ya  vijana  kuomba na mpaka kujiunga na jeshi hilo kwa kujitolea unaanza mwezi agosti 2020 na vijana watakaoteuliwa wanatakiwa waripoti kwenye makambi ya JKT  mwezi Oktoba 2020.

“Jeshi la kujenga Taifa linapenda kuwataarifu vijana kuwa watakaopata  fursa hiyo kuwa halitoi ajira kwa vijana na pia halihusiki na kuwatafutia vijana ajira katika asasi, vyombo vya ulinzi na usalama na mashirika mbalimbali  serikali na yasiyo ya serikari bali hutoa mafunzo ambayo yatawasaidia vijana kujiajiri wenyewe mara tu wanapomaliza mkataba wao pale tu wanapomaliza mafunzo yao ya Jeshi la kujenga Taifa”

“Sifa za mwombaji  awe raia wa Tanzania elimu na umri ,vijana wenye elimu ya darasa la saba umri ni kuanzia miaka 16 hadi 18, na kwa vijana wenye elimu ya kidato cha nne  umri usiwe zaidi ya miaka 20 na kwa vijana  wa kidato cha sita umri usiwe chini ya miaka 18 na usiwe zaidi ya miaka 22 vijana wenye elimu ya stashahada umri usiwe zaidi ya miaka 25 na elimu ya  shahada usiwe zaidi ya miaka 26, na shahada ya uzamili usiwe zaidi ya 30, na shahada ya uzamivu umri usiwe zaidi ya miaka 35” alisema kanali Kadawi.

Amesema kutokana na ugonjwa wa homa kali ya mapafu [COVID 19] nchini tahadhali za kuzuia maambukizi ya ugonjwa huo kama zilivyoelekezwa na serikali kupitia wizara ya afya zitazingatia kwa kipindi chote vijana watakapokua makambini.

Hata hivyo  kanali  Kadawi ametoa wito kwa  vijana wote watakaopata  fursa  hiyo ya kujiunga  waitumie ili wajifunze uzalendo ukakamavu stadi za kazi na stadi za Maisha na pia  kuwa tayari kulinda na kulitumikia Taifa.
Share To:

msumbanews

Post A Comment: