Na.Mwandishi Wetu – Arusha
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Uwekezaji,Angellah Kairuki amesema kuwa serikali ya Awamu ya Tano,inaendelea kutengeneza Mazingira mazuri kwaajili ya Uwekezaji ili kuvutia sekta hiyo.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Uwekezaji,Angellah Kairuki amesema kuwa serikali ya Awamu ya Tano,inaendelea kutengeneza Mazingira mazuri kwaajili ya Uwekezaji ili kuvutia sekta hiyo.
Akizungumza jijini Arusha katika ziara yake ya kikazi ya siku mbili Kairuki alisema kuwa serikali chini ya raisi Daktari John Pombe Magufuli inaendelea kutengeneza mazingira rafiki na wezeshi ili Wawekezaji waendelee kutumia fursa Mbali mbali.
Akizungumza katika kiwanda Cha Kutengeneza Transfoma Cha Tanelec amewapongeza kwa kazi nzuri ambayo wanaifanya na kuwataka kuendelea kuongeza jitihada na kuhakikisha kuwa wanatumia malighafi za ndani ya nchi.
“Kiwanda Hiki Cha Tanalec Ni kiwanda kikubwa Sana,na kimeweza kuitangaza nchi katika bara la Afrika Ila niwaombe kuwa zipo malighafi ambazo mnaagiza nje ya nchi Sasa tujaribu kuhakikisha kuwa tunawasiliana na viwanda vingine kuona namna ya kupata Mali ghafi hapa hapa nchini,tuokoe hizo fedha za kigeni”alisema Kairuki
Alisema kampuni hiyo ambayo ni mbia na serikali inajitahidi kuhakikisha inatengeneza transfoma nyingi kwaajili ya kuwezesha Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) kusambaza umeme hadi kufikia Juni 29 mwaka huu serikali ya awamu ya tano imefanikisha kusambaza umeme kwa vijiji 9,314 ikilinganishwa na vijiji 2018 vilivyokuwa vimeunganishwa umeme kwa mwaka 2018 sawa na ongezeko la asilimia 361.5 kupitia mpango kabambe wa usmbazaji umeme vijijini
Alisema tangu Rais Magufuli alipoingia madarakani hadi leo hii wateja zaidi ya milioni 2.7 wamepata umeme sawa na ongezeko la asilimia 361.5 huku akiwasisitiza kuendelea kufanya tafiti za kimasoko ili kuona uhitaji wa transfoma mbalimbali katika nchi za EAC pamoja na nchi nyingine.
“Nawapongeza kwa kuzalisha transfoma hizi lakini endeleeni kuendelea kutengeneza transfoma na kupata masoko zaidi katika nchi za EAC pia fanyeni tafiti zaidi za masoko ili kuuza zaidi transfoma hizi zinazozalishwa Tanzania “
Mkurugenzi wa Tanelec, Zahir Saleh alisema kuwa wanalazimika kununua waya aina ya enamael kutoka nje ya nchi kwa gharama kubwa ingawa Tanzania kuna viwanda vinne vinavyotengeneza waya ila hawatengenezi waya aina hiyo ndio maana wanaagiza nje ya nchi.
Pia aliomba Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kuondoa urasimu wa kodi mbalimbali pale wanapoingiza bidhaa kutoka nje y nchi kwaajili ya kutengeneza transfoma nchini ni kuishukuru serikali kushirikiana kwa pamoja katika kuendesha kiwanda hicho kwani hivi sasa tangu kuanzishwa kwa viwanda vingi awamu hii ya tano wamiliki wa viwanda mbalimbali vilivyopo nchini wanaona mafanikio.
Naye Mkuu wa Wilaya ya Arusha, Kenani Kihongosi alimshukuru uwepo wa kiwanda hicho ikiwemo kusambaza transfoma zaidi katika miradi mbalimbali Rea iliyopo vijiji mbalimbali nchini na mijini.
Kenani alitumia muda huo kuwakaribisha Wawekezaji wote Wilaya Arusha na kusema kuwa Serikali mkoani Arusha bado itaendelea kuunga mkono jitihada za Serikali za kuhakikisha viwanda vinaongezeka ili kuongeza Ajira.
Post A Comment: