Na,Jusline Marco;Karatu
Zaidi ya dolla za kimarekani milioni 10 zimetolewa na Shirika la World Vision Tanzania katika kuendeleza miradi ya maendeleo inayotekelezwa katika Wilaya ya Karatu Mkoani Arusha chini ya shirika la KOICA.
Akizungumza katika uzinduzi wa mradi wa pamoja wa Afya na Maji na Mazingira(KIHEWA)Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Karatu Waziri Morisi amesema kuwa kipitia mradi huo vifo vya mama wajawazito na watoto vitaweza kupungua kwa kiwango kikubwa.
Awali akizungumza katika uzinduzi huo Mkurugenzi wa World Vision Tanzania,Gilbert Kamanga amesema kuwa mradi huo ni mradi jimuishi wa afya na maji katika eneo la Karatu ambapo ameishukuru serikali kwa kuweka mazingira wezeshi kwa mashirika binafsi ili yaweze kufanya kazi za kimaendeleo.
Ameongeza kuwa World Vision ni shirika ambalo linaangalia ustawi wa mtoto ambapo kupitia mradi huo wamelenga ni watoto walio chini ya miaka 5 ili waweze kunufaika kwa kupunguza vifo vya watoto na kuyokomeza vifo vya mama wajawazito wakati wa kujifungua.
"Tujitahidi kushirikiana ili tuhakikishe uwekezaji huu unaongezeka thamani kwa kuona matokeo ya kaya zinazonufaika kwani hela hizo ambazo zimewekezwa zinapaswa zitoe matokeo chanya katika kaya zetu na tuhakikishe kwamba kunakuwa na uwajibikaji na uadilifu katika rasilimali hizi ambazo tunazitumia"Alisisitiza Mkurugenzi huyo
Vilevile amewataka viongozi waliohudhuria uzinduzi huo kuwa sehemu ya jamii katika kusimamia na kitokomeza mila potofu ambazo zknawazuia watu kupata huduma bora za kiafya.
Kwa upande wake Meneja wa Mradi huo Flavian Ngeni amesema kuwa mradi huo ambao unatekelezwa kwa miaka 3 katika vijiji 10 kwenye karafa mbili za Endabash na Lake Eyasi na umelenga kutatua changamoto mbalimbali ambazo zipo katika maeneo ya tarafa hizo sambamba na kuhakikisha uwepo wa mazingira wezeshi ya utolewaji wa huduma bora za afya ya uzazi kwa mama na mtoto chini ya miaka 5 pamoja na vijana balee ili kuweza kupunguza vifo visivyo vya lazima.
Ameongeza kuwa katika utekelezaji wa mradi huo kwa mwaka wa kwanza wataanza na vijiji viwili vya Bassodawish na Mbunga nyekundu ambapo wanatazamia kuwa na wanufaika wa moja kwa moja wapatao elfu 11937,watoto walio chini ya miaka 5 elfu 9871 pamoja na wanawake wajawazito elfu 1000 huku katika mradi huo wanufaika wasio wa moja kwa moja wakiwa elfu 46545.
Pamoja na hayo Mganga Mkuu wa Mkoa wa Arusha Dkt.Wilson Sichalwe amesema kuwa serikali ya Mkoa imeendelea kuboresha na kuimarisha huduma za afya katika suala la upatikanaji wa dawa,vifaa tiba na vitendanishi kwenye vituo vya kutolea huduma.
Sambamba na hayo amewataka watendaji wa vijiji na viongozi wa dini kuhakikisha wananchi wanamiliki huduma zinazotolewa katika vituo vya afya kwa kuona afya ya uzazi inamuhusu mtu moja moja.
Post A Comment: