Mchakato wa kura za Maoni Majimbo saba ya mkoa wa Manyara umeenda vizuri ambapo uchaguzi ulifanyika kwa uwazi kila mgombea akisimamia kura zake.
Katika mchakato huo wapo wabunge waliomaliza muda wao na kubahatika kupata kura zitakazowawezesha kuingia kwenye Kinyang’anyiro cha uchaguzi baadaye Oktoba 28 mwaka huu.
Aliyekuwa Mbunge wa Babati Mjini kupitia Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Paul Gekul na baadae kurudi Ccm, ameshindwa kura za maoni kwenye Jimbo hilo kupitia CCM.
Gekul amepata kura 61, mshindi ni Esther Mahawe alieekuwa Mbunge wa viti Maalum mkoa wa Manyara ambaye amepata kura 91 akifuatiwa na aliewahi kuwa Mbunge wa Ccm jimboni hapo 2010-2015 Werema Chambiri mwenye kura 77.
Babati Vijijini, aliepita katika kura za Maoni Jimbo hilo ni Daniel Baran Sillo alieshinda kwa kupata kura za wajumbe 502 akifuatiwa na Mbunge alimaliza muda wake Jituson Vrajilal akivuna kura 68 na wa tatu akiwa Steven Manda kura aliepata 42.
Katika Jimbo la Simanjiro, aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Njombe Christopher Ole Sendeka ameongoza katika uchaguzi wa kura za maoni kwa kupata kura za wajumbe 309, akifuatiwa na Kiria aliyepata kura 47 na wa tatu ni Matei ambaye amepata kura 17.
Jimbo la Mbulu mjini aliekuwa Mbunge wa jimbo hilo Zacharia Paul Isaay ameongoza kwa kura 373, nafasi ya pili ikishikwa na Dk. Safari kwa kupata kura76 huku ya tatu ikishikiliwa na Vakeeian aliepata kura 13.
Aidha Matokeo ya kura za maoni ndani ya chama cha mapinduzi (CCM) jimbo la Mbulu vijijini aliekuwa Mbunge wa jimbo hilo Flatei Masay ameongoza kwa kupata kura 531, Dk. Emmanuel Nuwas kura 94 na wa tatu ni James Gitonge aliepata kura 11.
Kwa upande wa Hanang, alieyekuwa Mbunge wa jimbo hilo kwa Miaka 25 Dk. Mary Nagu, ametupwa nje katika kura za maoni kwa kupata kura 210 huku alieshinda mchakato huo George Bajuta , akiwa na kura 267 na wa tatu ni Samweli Hayuma akiuwa na kura 37.
Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) nchini Tanzania imesema, Uchaguzi Mkuu wa udiwani, ubunge na Urais wa Tanzania utafanyika Jumatano Oktoba 28, 2020.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam Jumanne Julai 21, 2020, Mwenyekiti wa NEC, Semistocles Kaijage amesema Uchaguzi mkuu utafanyika October 28 Mwaka huu huku Kampeni zikitarajiwa kuanza August 26 hadi October 27, 2020.
Post A Comment: