Mkuu wa Takukuru Mkoa wa Pwani Suzan Raymond akizungumza na waaandishi wa habari kuhusina na tukio hilo la kukwamatwa kwa mtuhumiwa kwa kosa la kupokea ruhswa kiasi cha shiloingi milioni 15.


TAASISI ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Mkoa wa Pwani immemburuza mahakamani Joseph Mwenda kwa tuhuma za kushawishi na kupokea Rushwa ya zaidi ya Shilingi milioni 15.kinyume na kifungu Cha Sheria ya Kupambana na Rushwa namba 11 ya mwaka 2007.

Mkuu wa Takuku  Mkoa wa Pwani Suzana Raymond  alibainisha hayo wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na tukio hilo.

Aidha Suzana alisema,  kwamba mtuhumiwa huyo alifanikiwa kupata fedha hizo kutoka kwa mwananchi kwa madai kuwa fedha hizo ziliombwa na Afisa wa TAKUKURU ili aweze kumsaidia mtuhumiwa huyo kwenye kesi yake.

Mkuu huyo wa Takukuru alisema, Taasisi hiyo ilipata taarifa kutoka kwa msamariamwema kuhusiana na anachokifanya Mwenda ndipo walipojipanga na kufanikiwa kumkamata.

Suzana alisema, uchunguzi dhidi ya mtuhumiwa huyo unaendelea ili kubaini malengo yake na watu ambao tayari amewatapeli.

Alitumia nafasi hiyo kuwaasa wananchi kutoa taarifa mara wanapopigiwa simu na mtu yeyote atakayejitambulisha kuwa ni Afisa wa TAKUKURU na kudai fedha au kutaka kuonana eneo ambalo sio ofisi ya Taasisi hiyo.

“Napenda kuchukua nafasi hii kupitia vyombo vya habari kuwaasa wananchi wote wa mkoa wa Pwani kuhakikisha wanatoa taarifa mara wanapopigiwa simu na watu wowote ambao waatajitambulisha kuwa wanafanya kazi katika ofisi ya Takukuru ili waweze kuchukuliwa hatua kali za kisheria.
Share To:

Post A Comment: