Na John
Walter-Babati
Taasisi ya
kuzuia na kupambana na rushwa mkoani Manyara imemfuta machozi Mwalimu mkuu
mstaafu wa shule ya Sekondari Galapo katika wilaya ya Babati aliedhulumiwa haki
yake kwa kutozwa riba ya asilimia mia tatu na kulazimika kulipa milioni
arobaini na mbili baada ya kukopa milioni kumi na nne .
Taarifa
iliyotolewa na mkuu wa Takukuru mkoa wa Manyara Holle Makungu,imeeleza kuwa
wakati Mstaafu huyo akisubiri mafao yake alikopa kutoka kwa wakopeshaji wa
mitaani jumla ya shilingi milioni 14 na alitakiwa kurejesha mkopo wote pamoja
na riba mara baada ya kupokea mafao yake ambayo ni asilimia 41 lakini
wakopeshaji hao walimlaghai akalipa asilimia 300.
Makungu
ameeleza kuwa kutoka kwenye mkopo wa shilingi milioni 14 walaghai hao
walijipatia shilingi milioni 42 ambapo kati ya fedha hizo wamefanikiwa
kumrejeshea mwalimu huyo shilingi Milioni 20.
Hata hivyo
mkuu wa Takukuru mkoa wa Manyara ametoa wito kwa wastaafu wenye shida ya mikopo
waachane na mikopo umiza mitaani na badala yake waende benki ya posta ambapo
matawi yake yameenea nchi nzima na benki zingine zinazokubali kutoa mikopo kwa
wastaafu.
Amesema hilo
likizingatiwa tatizo hilo la mikopo umiza haliwezi kuwepo tena hivyo kuisaidia
Takukuru kuendelea na majukumu mengine kama yalivyoanishwa na sharia ya kuzuia
na kupambana na Rushwa namaba 11/2007.
Kwa upande
wake Mwalimu mkuu msataafu Loth Isaac Ndaalu ameangua kilio kwa furaha mara baada ya kurejeshewa kiasi hicho cha fedha na
taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa mkoani Manyara zinazotokana na mikopo
kandamizi ambapo alitozwa riba ya
asilimia kubwa na kulazimika kulipa Zaidi ya makubaliano.
Mwalimu huyo
mstaafu ameishukuru Takukuru na serikali ya awamu ya tano kwa kufanikisha
kurudisha fedha hizo ambazo alishazipoteza.
Mwalimu huyo
mstaafu ameishukuru takukuru na serikali ya awamu ya tano kwa kufanikisha
kurudisha fedha hizo ambazo alishazipoteza.
Katika hatua
nyingine Makungu amesema katika kipindi cha mwezi april mpaka june mwaka huu,
Takukuru mkoani Manyara imefanikiwa kuokoa Milioni 147,897,612.00 ambazo
ziirejeshwa kutoka mikononi mwa watu wasiokuwa waaminifu huku sehemu kubwa ya
fedha hizo zikiwa ni za mikopo toka katika benki ya Kilimo Tanzania (TADB) .
Aidha kwa
upande wa uchunguzi wan a mshtaka,katika kipindi cha kuanzia april jadi juni
2020, TAKUKURU ilipokea jumla ya malalamiko 1305 ambapo kati ya malalamiko
hayo, 104 yalihusiana na makosa ya rushwa na malalamiko 31 yalihusu makosa
mengine ambapo walalmikaji walishauriwa na kuelekezwa katika ofisi husika kwa
ajili ya utatuzi wa malalmiko yao.
Makungu
ameongeza kuwa jumla ya kesi saba zilifunguliwa ambapo kesi nne zilihusu
halmashauri na viongozi wa serikali za vijiji, kesi mbili zenye jumla ya
washtakiwa wane zilihusu watumishi wa mamlaka ya mapato (TRA) kupokea rushwa,
na kesi moja ilihusu mwenyekiti na katibu wa Chama cha Mapinduzi tawi la
Maisaka Kati mjini Babati kujihusisha na vitendo vya rushwa.
Amesema kesi tano zilitolewa uamuzi ambapo washtakiwa
walipatikana na hatia na kupewa adhabu stahiki ikiwemo kesi CC.48/2016 ambapo
aliyekuwa mweka hazina wa halmashauri ya wilaya ya Simanjiro alihukumiwa miaka
saba gerezani ana ameshaanza kutumikia kifungo tangu Mei 7,2020.
Post A Comment: