Na John Walter-Manyara
Taasisi ya Kuzuia na Kupambana
na Rushwa (Takukuru), mkoa wa Manyara imewaomba watanzania kusaidia kutoa
taarifa zitakazosaidia kupatikana kwa
Mmiliki wa kampuni ya JACO SERVICES GROUP John Stepheni Kabelinde anaedaiwa
kutumia nyaraka feki kupata zabuni.
Taarifa
iliyotolewa na mkuu wa Takukuru mkoa wa Manyara Holle Makungu leo Julai 9.2020
imeeleza kuwa, mtu huyo anatuhumiwa kwa kujipatia kandarasi yenye
nambari za usajili TRD/RM/MYR/2019-20 toka Tanroads mkoani Manyara iliyohusu
kufyeka nyasi pembeni mwa bara bara inayotoka Babati hadi Gehandu wilayani
Hanang.
Makungu
amesema John Stepheni Kabelinde maarufu kwa jina la Babu Joha huonekana mara
kwa mara maeneo ya Sinza makaburini jijini Dar es Salaam ambapo inasadikika ndipo anapoishi na kuendesha
shughuli zake.
Ameongeza kuwa uchunguzi walioufanya unaonyesha kuwa
Babu Joha aliwasilisha nyaraka za kupotosha zilizomwezesha kuwashinsda wazabuni
wengine tisa walioomba kazi hiyo.
Amesema kuwa
mtuhumiwa huyo kupitia kampuni yake ya JACO SERVICES GROUP, amekuwa akikwepa kulipa kodi mbalimbali za
serikali hivyo kuangukia kwenye makosa ya kuhujumu uchumi wa taifa.
Ametoa rai
kwa wananchi wa mkoa wa Manyara na watanzania wote kupitia vyombo vya habari,
kwamba popote watakapomuona Babu Joha watoe taarifa katika ofisi za TAKUKURU
zilizopo karibu au kupitia namba ya
dharura 113 au kwa kamanda wa TAKUKURU
mkoa wa Manyara 0738150124-25
Aidha amezionya
kamati za tathmini katika Taasisi nunuzi kutimiza majukumu yao kwa kuhakiki
kila kampuni wanayoifanyia tathmini kuona uhalali wa nyaraka zilizowasilishwa
na kujiridhisha iwapo kampuni husika inalipa kodi za serikali kwani kushindwa
kufanya hayo ni matumizi mabaya ya madaraka kinyume cha kifungu cha 31cha
sheria ya kuzuia na kupambana na rushwanamba 11/2007 na kwamba hatua
zitachukuliwa dhidi ya wahusika.
Post A Comment: