Na Ahmed Mahmoud Arusha
Katibu Tawala wa mkoa wa Arusha Richard Kwitega amesema sensa ya takwimu za Kilimo mifugo na Uvuvi itakayofanyika kuanzia mwezi ujao taarifa itakazokusanywa itaonyesha hali halisi ya sekta ya kilimo nchini na kuiwezesha serikali kupanga sera mipango kuimarisha na kuboresha hali za wananchi.
Kwitega ameyasema hayo wakati akifungua mafunzo ya siku tatu ya wadadisi wa sensa ya kilimo mifugo na uvuvi ya mwaka 2019/20 kutoka mikoa ya kanda ya kaskazini yalioandaliwa na Ofisi ya Taifa ya Takwimu inayofanyika jijini Arusha.
Alisema kuwa kwa ujumla umuhimu wa kilimo unafahamika na takwimu hizo zitaonyesha jinsi sekta hiyo inavyochangia katika pato la taifa kwani mwaka 2019 sekta hiyo imechangia pato la taifa kwa asilimia 26.6 huku upande wa mauzo ya nje asilimia 24.3 ya fedha za kigeni ilipatikana.
Aidha alibainisha kuwa tafsiri ya takwimu hizo kuwa mwaka huo wakulima tulizalisha zaidi tukavuna zaidi na kuuza zaidi huku wafugaji walifuga zaidi wakauza zaidi na wakazalisha zaidi hivyo hatuna budi kujivunia mchango wetu kwa sababu tunachangia katika kukuza maendeleo tunayoyaona sasa.
Alisema kuwa Wakati tukielekea kwenye sensa ya kilimo Mifugo na Uvuvi ya mwaka 2019/20 hatuna budi kuwakumbusha na kusisitiza kuwa mafanikio niliyoyataja hapo awali yanatokana na matumizi ya matokeo ya sensa ya mwaka 2007/8 ambayo ilifanyika kwa ufanisi mkubwa kwa kuonyesha maeneo tuliofanikiwa na kupiga hatua kubwa maeneo yaliosogea kidogo na yenye changamoto nyingi ambayo hayakupiga hatua kabisa pamoja na mipango na sera tulizotumia kufanikiwa.
"Kama alivyoeleza awali mwakilishi wa Mtakwimu mkuu wa serikali mafunzo haya yatakuwa na sehemu mbili za nadharia na vitendo itahusu kujaza dodoso la wakulima wadogo na wakubwa pia dodoso la mashamba makubwa la jamii mbinu za udadisi na kutumia teknolojia mpya katika kukusanya Takwimu kwa matumizi ya vishikwambi kwa kufuta sheria ya Takwimu muwe makini wa kuchukuwa taarifa sahihi"
Aliwataka kuanzia sasa tunapoitisha vikao vyetu kuhakikisha kuwa ujumbe wa sensa uwe wa kudumu katika mikutano yetu na wananchi tuelimishe na kuhimiza kutoa ushirikiano kwa wadadisi wakati wote wa zoezi hili linapofanyika na kwa upande wa wananchi wajibu wao mkubwa ni kushirikiana na wadadisi kwa kujibu maswali kwa usahihi na ufasaha bila ya kuficha ukweli wa taarifa.
Awali akiongea wakati akimkaribisha Mgeni Rasmi kwa niaba ya Mtakwimu mkuu wa Serikali Afisa Takwimu Muandamizi kutoka Ofisi ya Taifa ya Takwimu Robert Kasililwa alisema kila mwananchi ashirikiane na wadadisi kutoa taarifa sahihi ili serikali iweze kupanga mipango ya maendeleo endelevu katika sekta ya kilimo itakayosaidia kuongeza wigo wa kupunguza umaskini wa wananchi.
Alisema mafunzo hayo kitaifa yalianza siku ya Jumamosi wiki iliyopita kwa jumla ya wadadisi 322 nchi nzima kupatia mafunzo ya matumizi ya teknolojia mpya ya ukusanyaji wa Takwimu kwa mfumo wa Vishikwambi na kuachana na mfumo uliopita wa matumizi ya karatasi unaogharimu fedha nyingi.
Alisema kuwa teknolojia ya kisasa ambayo itapunguza gharama za kukusanya na kuchakata takwimu kwa kiasi kikubwa sana tofauti na sensa ya mwaka 2007/8 ambayo ilitumia takribani bilioni 10 huku sensa hii ya mwaka 2019/20 ikitumia pungufu bilion 6 kwa pande zote za Muungano Aidha matumizi hayo ya teknolojia hiyo itarahisisha upatikanaji wa takwimu kwa muda mfupi na ubora zaidi tofauti na huko nyuma.
Post A Comment: