Mgombea Urais wa Zanzibar kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Dkt Hussein Mwinyi amesisitiza ushirikiano na mshikamano ndani ya chama hicho wakati huu wa kuelekea uchaguzi mkuu mwezi oktoba mwaka huu.
Amesema ushirikiano na mshikamano ndio utakaokiwezesha chama hicho kupata ushindi wa kishindo katika uchaguzi mkuu ujao kwa pande zote mbili za muungano.
Dkt Mwinyi ameyasema hayo jijini Dodoma mara baada ya kutangazwa mshindi kwa kupata kura 129 kati ya kura zote zilizopigwa na wajumbe wa halmashauri kuu ya CCM Taifa jijjni Dodoma.
Dkt Mwinyi amewashinda Shamsi Vuai Nahodha aliyepata kura 16 na Dkt Khalid Salim Mohamed aliyepata kura 19.
Post A Comment: