Nguvu za kiume huhusisha mambo mengi. Yani pamoja na, hamu ya mapenzi; kusimama kwa uume barabara; kuchelewa kufika kileleni kiasi cha kufurahia tendo la ndoa; uwezo wa kurudia tendo la ndoa; pumzi, wepesi na uchangamfu wa mwili katika kutenda tendo lenyewe. Kuna viungo vingi mwilini vinavyohusika na nguvu za kiume.
Viungo hivi ni kama ubongo, moyo, mishipa ya neva mishipa ya ateri, mirija iliyo ndani ya uume iitwayo corpora cavernosa na kadhalika. Kukosa nguvu za kiume ina maana kuwa kiungo kimoja kati ya viungo vyote husika hakifanyi kazi kwa mfano figo yaweza kukosa kufanya kazi hivi basi kusababisha kukosa nguvu za kiume.
Kuna mambo kadhaa yanayosababisha ukosefu wa nguvu za kiume kwa mfano kupatwa na maradhi, vyakula unavyokula na mtindo wa maisha huweza kufanya viungo kutofanya kazi. Baadhi ya maradhi hayo ni ugonjwa wa sukari, presha ya kupanda, presha ya kushuka.
Tabia zinazosababisha viungo kutofanya kazi ni kama uvutaji wa sigara, kuchelewa kulala, kutopata usingizi, kujinyanyua, unywaji wa pombe, utumiaji wa madawa ya kulevya au kufanya kazi kupita kiasi hivi basi kukosa wakati wa kupumzika. Sababu nyingine ni kama kutumia nguvu nyingi kusukuma choo kwa sababu ya tatizo la kusukuma choo, kutokunywa maji, uzito mwingi, kitambi na hasa kutofanya mazoezi.
Kuna njia nyingi za kuongeza au kurejesha nguvu zako za kiume kwa mfano unaweza kubadilisha vyakula unavyokula kama kula nafaka zilivyo na nyuzi nyuzi kwani nafaka husaidia kuongeza homoni za kiume, kula asli, kula matunda mengi, kula tangawizi, kunywa vanilla na kunywa maji mengi.
Njia nyingine ni kumtembelea datary na kumwambia shida yako, anaweza kukupa tembe au akudunge sindano kama njia ya kukusaidia njia ya mwisho na ambayo tunazungumzia ni kufanya mazoezi ambayo husaidia uongeza nguvu za kiume. Kati ya njia hizo zote hakuna ambayo utapata matokeo yake kwa siku moja, utahitaji kufuatilia njia hiyo na kuwa na uvumilivu na imani kuwa utasaidika mwishowe.
Kuna mazoezi mengi ambayo husaidia kurejesha nguvu za kiume kwa mfano:
1- Kujiinua pande ya juu ya mwili
Zoezi hili huhitaji uweke mpira wa zoezi chini na uwekelee mguu wako juu yake huku ukitumia mikono yako hushikilia upande wa juu wa mwili wako.
Hujaribu kuonyesha kuwa unapoweza kushikilia mwili wako kwa muda mrefu basi utaweza kuongeza nguvu zako za kiume zaidi. Sehemu ya mwili inayoongezwa misuli ni mabega, kifua na upande wa mbele wa mkono pande juu.
2- Kujiinua pande ya chini ya mwili
Aina hii ya zoezi inahitaji ulale wima kwa mgongo kasha uinue miguu yako hadi kwenye kifua na kisha ushikee miguu yako kutoka nyma kwa sekunde thelathini.
Rudia jambo hili kwa mara nyingi kama utakavyoweza. Husaidia sehemu ya chini ya mgongo na kutengeneza misuli ya tumbo.
3- Pande ya chini ya mwili
Zoezi hili unafaa kupiga magoti na kuweka sehemu ya juu ya mwili wima kasha unafaa kuinamisha sehemu ya juu ya mwili pole pole huku ukiinama zaidi hadi mahali ambapo utashindwa kurudi nyuma zaidi.
Kaa hivyo kwa sekunde thelathini kisha upumzike na kurudia zoezi hili kwa mara kadhaa. Zoezi hili husaidia kuongeza misuli sehemu ya juu ya miguu.
4- Kuongeza nguzu sehemu ya kati ya mwili
Katika zoezi hili unafaa kusimama huku ukiwa umerudisha mguu moja nyuma na mwingine mbele na kuinamisha sehemu ya juu ya mwili nyuma.
Miguu inafaa kuwa na tofauti ya mita moja na kiuno kinafaa kuwa umekisukuma mbele. Baada ya dakika moja geuza miguu. Zoezi hii husaidia kuongeza misuli ya kiuno.
5- Uvumilivu
Zoezi hili hufanywa kama umelala kwa mgongo huku umekunja miguu yako na mikono ikiwa wima pande zote za mgongo.
Kisha uinue kiuno na kukaa hivyo kwa dakika kadhaa, zoezi hili husaidia kupima uvumulivu wako ukiwa umeinua kiuno na kusaidia kuongeza nguvu katika kiuno chako.
6- Kuinua uzito
Kuinua vitu vyenye uzito ni aina ya zoezi inayosaidia kuongeza nguvu za kiume. Zoezi ya aina hii husaidia mtu kujiamini kwa chiochote anachofanya hata anapoinua vitu hivyo vyenye uzito.
Kuinua kwa vitu vizito kama mawe husaidia kuongeza misuli mikononi hasa upande wa juu, upande wa mbele. Misuli hio husaidia kuongeza nguvu mwilini.
7- Kutembea
Hii ni aina rahisi ya zoezi ambayo haihitaji matumiizi ya nguvu nyingi lakini watu wengi hawapendi zoezi hili. Badala yake watu hupenda kuendesha magari ili wasichoke.
Kutembea husaidia kupunguza uziti na kitambi. Vile vile kutembea husaidia kupunguza uchovu baada ya kufanya kazi ambayo haihitaji nguvu nyingi.
8- Kuchuchumaa
Hii ni aina ya zoezi ambayo unahitaji kuekelea mikono yako kwenye kiuno chako na kuchuchumaa hadi chini ambapoutakua umekalia miguu yako na kuinamka bila ya kuondoa mikono kutoka kwa kiuna na bila kuondoa miguu mahali ilipo.
Zoezi ya aina hii husaidia kuongeza nguvu na misuli pande ya nyuma ya miguu ili kuweza kushikilia mwili.
9- Kuruka
Kuruka ni zoezi nzuri kwa kuongeza nguvu za kiume. Unaporuka unaongeza miguu yako nguvu na misuli kwani unapoondoa mwili juu unahitaji kusimama au kujishikilia vizuri ili usianguke.
Mazoea ya kuruka huhakikisha miguu ina nguvu ambalo ni jambo la muhimu sana katika uongezaji wa nguvu za kiume.
10- Kuogelea
Kuogelea ni tendo la kuingia katika maji mengi na kutoka mahali pamoja hadi pengine bila ya kutembea. Kuogelea husaidia mikono na miguu yao.
Unapoogelea misuli ya miguu na misuli ya mikono yako huongezeka, nguvu vako mwilini huongezeka kwani unatumia mwili wote katika kuogelea. Miguu husonga na mikono vile vile hivi basi mishipa ya damu lazima ipeleke damu nyingi mikononi na miguuni.
11- Kutembea kwa haraka
Hii ni tofauti na kukimbia na pia ni tofauti sana na kutembea. Kitu cha muhimu kujua ni kuwa unahitajika kutenganisha miguu yako kwa mbali na kwa haraka.
Unapotenganisha miguu na kutembea kwa haraka misuli ya upande wa juu wa mguu inaongezeka na pia mishipa ya damu inasafirisha damu upande wako wa juu wa mguu. Hili ni jambo la muhimu sana kwani maana moja ya nguvu za kiume ni kuweza kusimama kwa uume barabara na ili uume usimame unahitaji damu kuwepo.
12- Kulala
Hii si aina ya zoezi lakini ni muhimu kwa mazoezi niliyoyataja hapo awali. Usingizi husaidia kupumzisha mwili pamoja na viungo vyote vya mwili. Kupumzisha mwili ni muhimu ili wakati ambapo unahitaji kufanya chocho uwe na nguvu zinazofaa.
Post A Comment: