Mkuu wa wilaya Hai lengai ole sabaya amemshukuru  Rais wa Jamuhuri wa Mungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli kwa kumwamini miongoni mwa watanzania wengi na kumteua kuwa mkuu wa Wilaya ya Hai mkoani Kilimanjaro ameyasema hayo leo katika ibada ya shukrani iliyofanyika katika  kanisa la KKKT usharika wa sambasha ambapo ni nyumbani alipozaliwa mkuu huyo wa wilaya.

Dc Sabaya ameeleza kuwa haikuwa kazi raisi kuaminiwa na mkuu wa nchi na kumteua kwenda kuongoza wilaya ya Hai ni Eshima kubwa kwake na wananchi wa kata ya sambasha wilayani Arumeru .

Katika ibada hiyo ya shukrani Ole Sabaya aliongozana na viongozi mbalimbali wa chama cha mapinduzi Mkoa wa Arusha akiwemo Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Ccm Ndugu Omary Lumato,Meya mstaafu wa Jiji la Arusha Kalist Lazaro sambamba na mwanasheria nguli Charles Adiel.

Katika ibada hiyo ya shukrani Mkuu hiyo wa wilaya Lengai ole sabaya amechangia kiasi cha shilingi milioni kumi kwa ajili ya ujenzi wa kanisa akisema kuwa ni shukrani yake kwa mwenyezi Mungu baada ya kumaliza kuwatumikia wananchi wa sambasha kama Diwani wao.

Hata hivyo katika kipindi hiki cha uchaguzi mkuu Ole sabaya Ameeleza kuwa hatagombea nafasi yoyote na ameridhika na kazi aliyopewa na muheshimiwa Rais Magufuli.

Awali katika ibada hiyo Meya mstaafu wa Jiji la Arusha Kalist Lazaro akitoa salamu kwa waumini wa kanisa hilo aliwapongeza kwa kumchagua lengai ole sabaya kuwa diwani wao ambaye alifanya kazi kwa bidii kwa kuwatumia wananchi wa sambasha hadi Rais Magufuli alipompa fursa ya kwenda kuwatumia wananchi wa Hai.

Kalist ameeleza kwamba katika wakuu wa wilaya wote nchini wenye umri mdogo Dc sabaya ameonyesha mfano wa kuigwa kwa kufanya kazi kwa bidii kwa kutatua migogoro mbalimbali ya ardhi na kusimamia ujenzi wa miradi inayotekelezwa na serikali ya awamu ya tano ikiwemo Shule,Hospital,Barabara, pamoja na ujenzi wa jengo jipya la Ofisi ya mkuu wa Wilaya ya hai.

Kalist amewaeleza waumini hao kwamba Rais John Pombe Joseph Magufuli amemteua mtu sahihi ambaye anaendana na kasi ya serikali ya awamu ya tano hivyo waumini hao waendelee kumuombea Ole sabaya ili aendelee kuwatumikia vyema wananchi wa Hai bila kusahau kuendelea kumuombea Rais Magufuli.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa chama cha Mapinduzi mkoa wa Arusha Ndugu Omary Lumato ametoa rai kwa viongozi vijana wanaopata fursa za uteuzi kufanya kazi kwa bidii na kumtanguliza Mwenyezi mungu.

Lumato ameeleza kuwa sabaya alipitia changamoto kubwa ikiwemo kufunguliwa Kesi lakini hakukata tamaa aliendelea kuwatumikia vyema wananchi sambasha mpaka alipopata fursa ya kwenda kuwatumikia wananchi wa Hai.

Kwa upande wake mwinjilisti wa Mtaa wa sambasha Clement Kivuyo amempongeza na kumshukuru Lengai Ole sabaya kwa kufanya ibada ya shukrani iliyoambatana na mchango wa  kiasi cha shilingi Milioni kumi kwa ajili ya kumalizia ujenzi wa kanisa la Mtaa huo.

Mwinjilisti Kivuyo amesema kwamba DC sabaya  amefanya kitu kizuri kutoa shukrani kwani baadhi ya viongozi wa serikali huwa wakishapata vyeo huwa wanajisahau na kukaa mbali na jamii inayowazunguka.

Mwanasheria Ngoli Charles Adiel amesema wamejitokeza kumsindikiza mkuu huyo wa wilaya kutoa shukrani  pamoja na kutoa mchango wa kumalizia ujenzi wa kanisa na kuwataka viongozi kujituma katika kusaidia taasisi za dini.


Share To:

Post A Comment: