MWENYEKITI wa Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi na Mjumbe wa Kamati kuu ya Halmashauri kuu ya CCM, Ndg Kheri James ameendelea na  ziara ya kikazi ya Kuzungumza na Viongozi wa CCM pamoja na Jumuiya zake juu ya maandalizi ya Uchaguzi pamoja na mambo mengine Ame kagua Utekelezaji wa Ujenzi wa Nyumba za Watumishi wa UVCCM  Mkoa wa Singida.

Katika Ziara hiyo Ndg Kheri ameweka jiwe la Msingi katika Ujenzi wa Nyumba Ya Katibu wa UVCCM Wilaya ya Manyoni pamoja na Kukagua maendeleo ya Ujenzi wa Nyumba ya Katibu wa UVCCM Wilaya ya Ikungi.

Akizungumza na Wajumbe hao Kwa Nyakati Tofauti Ndg kheri Amewataka Viongozi hao Kuendelea  kupeana Ushirikiano katika kutekeleza Majukumu Yao kwa Kuzingatia Taratibu,Miongozo ,Kanuni pamoja na Katiba ya Chama Cha Mapinduzi.

Pia Komred kheri amesisitiza Viongozi hao kutumia muda hu kuimarisha Umoja na Mshikamano na Kuepuka Migogoro itakayo vunja Umoja na Mshikamano wa Chama Cha Mapinduzi.

Akizungumza na Viongozi hao kuelekea Katika Uchaguzi Mkuu Ndg Kheri amewasisitiza Viongozi hao kujiepusha na Vitendo mbalimbali Vya Rushwa kwa Chama ili kuwapa fursa Wanachama mbalimbali fursa za kugombea katika nafasi mbalimbali.

Katika Ziara hiyo Ndg Mwenyekiti aliongozwa na Mwenyeji wake Mwenyekiti wa UVCCM Mkoa wa Singida Dkt Denis Nyiraha,Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa,Katibu wa Chama Cha Mapinduzi Mkoa Pamoja na Wajumbe wa Kamati ya Siasa na Utekelezaji Mkoa.

Ndg Mwenyekiti amehitimisha Ziara yake leo katika Wilaya ya Manyoni na Ikungi na kesho ataendelea  na Ziara katika Wilaya za Singida Mjini na Vijijini.


Share To:

Post A Comment: