Katibu
Mkuu Wizara ya Kilimo, Gerald Kusaya,akizungumza wakati wa kikao cha
Makamishna na watumishi wa Tume ya Maendeleo ya Ushirika kilichofanyika
Jijini Dodoma.
Katibu
Mkuu Wizara ya Kilimo, Gerald Kusaya,akisisitiza jambo kwenye kikao cha
Makamishna na watumishi wa Tume ya Maendeleo ya Ushirika kilichofanyika
Jijini Dodoma.
Mwenyekiti
wa Tume ya Maendeleo ya Ushirika Dkt. Titus Kamani,akitoa neno kwenye
kikao cha Makamishna na watumishi wa Tume ya Maendeleo ya Ushirika
kilichofanyika Jijini Dodoma ambapo mgeni rasmi alikuwa Katibu Mkuu
Wizara ya Kilimo, Gerald Kusaya.
Mrajis
wa Vyama vya Ushirika na Mtendaji Mkuu wa Tume ya Maendeleo ya Ushirika
Dkt.Benson Ndiege,akitoa taarifa wakati wa kikao cha Makamishna na
watumishi wa Tume ya Maendeleo ya Ushirika kilichofanyika Jijini Dodoma
ambapo mgeni rasmi alikuwa Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo, Gerald Kusaya.
Afisa Ushirika Mkuu Bi.Veneranda Mugoba,akitoa neno la shukrani kwa
mgeni rasmi Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo, Gerald Kusaya mara baada ya
kumaliza kikao cha Makamishna na watumishi wa Tume ya Maendeleo ya
Ushirika kilichofanyika Jijini Dodoma
Sehemu
ya Watumishi wa Tume ya Maendeleo ya Ushirika wakifatiliwa Hotuba ya
Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo, Gerald Kusaya wakati wa kikao cha
Makamishna na watumishi wa Tume ya Maendeleo ya Ushirika kilichofanyika
Jijini Dodoma
.............................................................................................
Na.Alex Sonna,Dodoma
Katibu
Mkuu Wizara ya Kilimo, Gerald Kusaya ameipongeza Tume ya Maendeleo ya
Ushirika Tanzania (TCDC) kwa kuendelea kuimarisha na kuendeleza Sekta ya
Ushirika nchini katika Nyanja za Kilimo, ufugaji, uvuvi, madini kwani
sekta hizo zimeendelea kuchangia uchumi wa Taifa.
Umuhimu wa Sekta hizo umetokana na kuwaunganisha wanachama katika uzalishaji, ukusanyaji mazao na upatikanaji wa masoko.
Kauli hiyo ameitoa wakati wa kikao cha Makamishna na watumishi wa Tume ya Maendeleo ya Ushirika kilichofanyika Jijini Dodoma.
Kusaya
amesema kuwa Serikali kupitia Tume ya Maendeleo ya Ushirika imefanya
na inaendelea na jitihada mbalimbali za kuimarisha Ushirika nchini.
Serikali
imejikita katika kuimarisha Usimamizi na Utawala Bora katika Vyama vya
Ushirika, kupitia Sheria ya Ushirika Na 6 ya Mwaka 2013 na Kanuni za
mwaka 2015.
Aidha
Kusaya amesema kuwa usimamizi wa vyama unaanzia kwa mwanachama
mwenyewe, juhudi zimeelekewa kwenye Mafunzo kwa viongozi wa vyama vya
ushirika na wanachama wao kupitia mpango kazi uliotolewa naTume ya
Maendeleo ya Ushirika.
Pia serikali imeendelea kuchukua hatua kupitia vyombo vya usalama pale ambapo kuna wizi na ubadhilifu kwenye vyama.
Nia ya serikali ni kurudisha Imani ya wananchi juu ya ushirika.
“Kwa
hatua hizi kumekuwepo na mabadiliko chanya kwenye ushirika ambapo
wananchi wameendelea kuanzisha na kujiunga katika vyama vya Ushirika wa
aina mbalimbali ikiwemo vyama vya Ushirika wa Kilimo na Masoko (AMCOS)
hatua ambayo itawezesha kupanua shughuli zao za uzalishaji mali na
kuongeza kipato na hatimaye kupunguza umasikini.
Pia,
kwa sasa wakulima wanauza mazao yao kupitia mfumo wa Ushirika. Mfumo
ambao umesaidia kuimarisha ubora wa mazao, kupatikana kwa bei za
ushindani, uhakika wa vipimo vya mazao,” alisistiza Bw.Kusaya
Mfumo wa Ushirika umesaidia upatikanaji wa takwimu sahihi za uzalishaji na uhakika wa mapato ya Halmashauri za Wilaya husika.
Kwa
kushirikiana na Soko la Bidhaa(TMX) na bodi za mazao, masoko ya mazao
ya kimkakati na mazao mchanganyiko yameendelea kuimarika kama vile
mazao ya tumbaku, choroko, kahawa, pamba, ufuta, kokoa na mbaazi
yaliuzwa kupitia mfumo wa ushirika katika msimu wa 2019/20 kwa thamani
ya Shilingi trilioni 2.7.
Awali
akiwasilisha Mafanikio na changamoto za Tume, Mrajis wa Vyama vya
Ushirika na Mtendaji Mkuu wa Tume ya Maendeleo ya Ushirika, Dkt. Benson
Ndiege, ameeleza kuwa Vyama vyama vya Ushirika wa Akiba na Mikopo
(SACCOS) vimeongeza mikopo kwa wanachama wake kutoka Shillingi Billioni
854 mwaka 2017 hadi kufikia Shillingi Trillioni 1.5 mwaka 2019 sawa na
ongezeko la asilimia.
Ushirika
ni Sekta ambayo imekuwa na mchango mkubwa katika kutoa ajira kwa vijana
na wananchi kwakuwa ni sekta ambayo inagusa maisha na uchumi wa mtu
mmoja mmoja na Taifa kwa ujumla.
“Tume
imeendelea kusimamia masuala ya ajira na kuwezesha wananchi Zaidi ya
90,090 kupata ajira katika vyama vya Ushirika zikiwemo ajira za kudumu,
mkataba na za msimu hadi kufikia Juni 2020 ikilinganishwa na ajira
32,668 mwaka 2018,” alisema Dkt. Ndiege
Kwa
upande wake Kamishna Salome Tondi, amesema Sekta ya Ushirika inaweza
kuendelea kukua na kuimarika kwa kuhakikisha elimu ya Ushirika
inawafikia wengi katika jamii.
Tondi
alifafanua kuwa elimu ni moja ya nyenzo muhimu inayoweza kuwakomboa
wanaushirika akitoa mfano wa masuala ya haki na wajibu wa wanaushirika,
taratibu za uendeshaji wa Vyama vya Ushirika, taratibu za uchaguzi wa
viongozi wa Vyama vya Ushirika na masuala mengine mengi.
Pamoja
na mambo mengine, kikao hicho kilikuwa ni fursa ya Makamishna kukaa kwa
pamoja na watumishi wa Tume kufanya tathmini ya masuala mbalimbali ya
Ushirika katika kipindi cha miaka mitatu kuanzia mwaka 2017 baada ya
uteuzi wao kwa mujibu wa Sheria ya Vyama vya Ushirika Na.6 ya mwaka
2013.
Post A Comment: