Sehemu ya waandishi kutoka vyombo mbalimbali Jijini Tanga wakichukua taarifa kwenye mkutano huo
Sehemu ya waandishi kutoka vyombo mbalimbali Jijini Tanga wakichukua taarifa kwenye mkutano huo
NA MWANDISHI WETU,TANGA.
DIWANI wa Kata ya Duga Jijini Tanga (CUF) Khalid Rashid amechukua fomu ya kuomba chama hicho kumteuwa kukiwakilisha chama hicho kwenye nafasi ya Ubunge kwenye Jimbo la Tanga wakati wa Uchaguzi mkuu utakaofanyika mwezi Octoba mwaka huu hapa nchini huku akieleza namna atakavyosaidia kuinua sekta ya elimu.
Akizungumza na waandishi wa habari leo Khalid alisema kwamba baada ya kuwatumikia wananchi wa Kata ya Duga kwa kipindi cha miaka mitano sasa anaona fursa pana ya kuwatumikia wananchi wa Jimbo la Tanga ili kuweza kurahisisha kasi ya maendeleo.
Alisema ingawa ni maamuzi mazito lakini ameamua kuyafanya na matumaini yake makubwa ni kwamba anaamini wana Tanga wanahitaji mbunge mpya ambaye atasaidia kusukuma gurudumu la maendeleo kwa wananchi na kuwaondolea changamoto zinazowakabili.
“Ndugu zangu waandishi wa habari leo nimewaita hapa kuna jambo nataka kuzungumza nanyi leo ni siku muhimu sana kwangu katika harakati za kiasiasa…siku zote nimekuwa nikitambulika kama diwani wa kata ya Duga na nitaendelea kubaki hivyo mpaka uchaguzi utakapofanyika”Alisema
“Lakini kuna kitu kimenisukuma rasmi akili yangu imenituma nifanye hivyo na nimewaita kuja kuwaambia tupo kwenye kipinbdi cha uchaguzi mkuu…kwa sababu tupo kwenye kipindi hicho CUF imetoa ratiba na maelekezo kila mwanachama kwenye nia ya kuwania nafasi hivyo mimi nimejitokeza kwenye chama kuichukua fomu kukiomba kiniteue kuwa mgombea wa Jimbo la Tanga “Alisema
Aidha alisema amejitathimini na kujitafakari akaamua kuchukua fomu na kujaza na tayari alikwisha rudisha ambapo amekiomba chama hicho kimteuwe awe mwakilishi wao kwenye Jimbo la Tanga kuipeperusha bendara.
Hata hivyo alisema kwamba ni matumaini yake kwamba CUF katika hili watatenda haki kumchagua mtu sahihi na wakati sahihi huku akieleza kwamba iwapo atakapata ridhaa hivyo atahakikisha anapambana kuhakikisha Jimbo hilo linapata mafanikio.
“Lakini mambo yaliyonisukuma ni mengi kwani nimekuwa diwani miaka mitano kuna mambo nimeyaona hivyo ndio maana natafuta fursa pana ya kuweza kuwasemea watu wa Tanga kupitia Bunge kwani kuna mambo bado yanakwenda kwa taratibu na ndio maana dhamira yake kuyasukuma yaende haraka haraka”Alisema
Hata hivyo alisema kwamba malengo yake ni kuhakikisha kwamva elimu inaimarika na kuwa na mafanikio kwa sababu elimu ndio msingi wa ukombozi wa kila mtanzania anataka kwenda kusimamia suala hilo kwa kuhamasisha wananchi.
Post A Comment: