KATIBU wa CCM Mkoa wa Tanga Shaibu Akwilombe akizungumza wakati wa mkutano wa Baraza  kuu la Jumuiya ya Wazazi wilaya ya Tanga kushoto ni Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi wilaya ya Tanga Nassoro Makau
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi wilaya ya Tanga Nassoro Makau akizungumza wakati wa mkutano huo kulia ni Katibu wa CCM Mkoa wa Tanga Shaibu Akwilombe
Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Tanga Meja Mstaafu Mkoba akizungumza kushoto ni Katibu wa CCM Mkoa wa Tanga Shaibu Akwilombe na kulia ni Katibu wa CCM wilaya ya Tanga


MBUNGE wa Viti Maalumu Mkoa wa Tanga na Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto Ummy Mwalimu akizungumza wakati wa kikao hicho
 MBUNGE wa Viti Maalumu Mkoa wa Tanga na Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto Ummy Mwalimu katika akiwa na Mwenyekiti wa Kamati ya Utekelezaji ya UWT wilaya ya Tanga Sussan Uhinga


Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Tanga (CCM) na Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto Ummy Mwalimu akiwa kwenye picha moja na Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi wilaya ya Tanga Nassoro Makau na Mwenyekiti wa UWT wilaya ya Tanga Moza Shilingi
 wakiwa kwenye ;picha ya pamoja

BARAZA kuu la Jumuiya ya Wazazi wilaya ya Tanga limempongeza Rais Dkt John Magufuli kwa uongozi bora wenye uweledi na kusimamia maadili kwa watumishi wa umma huku wakieleza kwamba anastahili kuendelea kuwatumikia watanzania.


Akizungumza katika kikao hicho Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi wilaya ya Tanga Nassoro Makamu alisema kwamba Rais Magufuli amefanya kazi kubwa iliyotukuka ya kuhakikisha anawapa maendeleo watanzania hivyo wataendelea kumuunga mkono kuelekea kwenye uchaguzi mkuu.


Alisema kwamba tarehe 14 ndio siku ya kuchukua fomu ua kuwania nafasi za udiwani na Ubunge na baadae uchaguzi huu lengo la chama na nia ya dhati  kwa kauli ya wazazi ni kumuhakikishia kura nyingi Rais Magufuli kwa mkoa wa Tanga kwa asilimia 98 .


Alisema kwani wao kama wazazi ni jeshi kubwa kwa sababu katika jumuiya hii vijana wapo, uwt wapo hivyo hawana sababu ya kuacha kumpa kura zote Rais Dkt Magufuli kwa wakati wa uchaguzi mkuu ambao unatarajiwa kufanyikamwezi Octoba mwaka huu.


“Ndugu zangu tunakwenda kwenye uchaguzi sisi kama wazazi tuhakikisha tunampa kura za ndio Rais Dkt Magufuli kwa asilimia 98 huku 78 zikitoka kwa wazazi na hatutashindwa kufanya hivyo kwa sababu wazazi ndio wenye kutafsiri elimu ya malezi kuelekea uchaguzi mkuu wa mwaka 2020”Alisema


Awali akizungumza wakati akifungua mkutano huo Katibu wa CCM Mkoa wa Tanga Akwilombe aliwataka kwenda kuitafsiri dhana ya elimu ya malezi kuelekea kwenye uchaguzi mkuu maana ya moja ya mambo yanayowapa changamoto ndani ya chama ni ukosefu wa elimu ya siasa na elimu ya utambuzi.
 “Tatizo lenu kubwa ni kuitafsiri dhana ya elimu na malezi kwa mujibu wa wakati… kuna jambo ambalo linazungumzwa sana ni uchaguzi tukiwa kwenye maandalizi ya mchakato ndani ya chama hivyo niwaombe muitafsiri dhana ya elimu na malezi kuelekea kwenyue uchaguzi mkuu “Alisema


Alisema kwa maana moja ya mambo yanayowapa changamoto ndani ya chama ni ukosefu wa elimu ya siasa na elimu utambuzi kwa kuwa jumuiya ndio ina dhamana ya kusimamia masuala ya elimu na malezi naomba jumuia ya wazazi Tanga mjini muitafisiri dhana ya elimu na malezi wakati chama kikielekea kwenye uchaguzi mkuu wa nchi.
Share To:

TANGA RAHA BLOG

Post A Comment: