Na Mwandishi Wetu Dodoma
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu amewataka wazazi kuwasimamia watoto katika matumizi ya vifaa vya keletroniki ili kuwaepusha kujiingiza katika vitendo vya ngono na ukatili mwingine mitandaoni.
Ameyasema hayo leo jijini Dodoma tarehe 15/06/2020 wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu maadhimisho ya Siku ya Mtoto wa Afrika yanayoadhimishiwa Juni 16 kila mwaka.
Ameongeza kuwa katika kipindi hiki tumeshuhudia watoto wanatumia vifaa ya kielektroniki ikiwa pamoja na simu na komputa kujifunzia, ni vyema watoto wazingatie matumizi sahihi ya vifaa hivyo ili kuepusha kufanyiwa vitendo vya kikatili.
Amesisitiza kuwa Wazazi au Walezi hakikisheni watoto Usalama wa watoto ni muhimu wakati wote na hivyo, watoto wakiwa nyumbani katika kipindi hiki wajiepushe kwenda kwenye maeneo yatakayo hatarisha usalama wao, ikiwa pamoja na kubakwa, kulawitiwa, kushawishiwa kufanya ngono na hata kupata maambukizi ya Corona.
“Katika eneo la malezi ya watoto wetu bado kuna changamoto kubwa ya matumizi ya mitandao tuhakikishe tunawasimamia waotto wetu wasijiingize katika masuala yasiyofaa katika mitandao hiyo” alisema.
Aidha Waziri Ummy amaesema kumekuwa na ongezeko la matukio ya vitendo vya ukatili wa kijinsia nchini ikiwa ni kwasababu wananchi wengi wamepata uelewa na kuweza kutoa taarifa katika maeneo maalum yaliyotolewa na Serikali kutoa taarifa hizo.
Ameitaja Mikoa ya kipolisi iliyoongoza kuwa na matukio mengi zaidi ya ukatili dhidi ya watoto kwa mwaka 2018 kwa ni Mkoa wa Tanga (1,039), Mbeya (1,001), Mwanza (809) na Arusha (792) na kwa mwaka 2019 ni Mkoa wa Tanga (matukio 1,156), Mkoa wa Kipolisi-Temeke (844), Mbeya (791) na Mwanza (758).
Kwa upande wake Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Maendeleo ya Mtoto Sebastian Kitiku amesisitiza wazazi kuwajibika kwa kuhakikisha wanawasimamia watoto wako kwa kuhakikisha wanawasimamia na kufuatilia masuala ambayo yanaweza kusababisha ukatili kwa watoto.
“Wazazi tuwaangalie watoto wetu tusiwaache watoto wakajiamulia baadhi ya vitu ambavyo vitawasababisha waingie katika mambo ambayo yatapelekea kufanyiwa vitendo vya kikatili” alisema.
Maadhimisho ya Siku ya Mtoto wa Afrika kwa mwaka 2020 inaoongozswa na Kauli mbiu isemayo “Mifumo Rafiki ya Upatikanaji Haki ya Mtoto: Msingi Imara wa Kulinda Haki Zao”
Post A Comment: