Na John Walter-Babati
Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Mkoa wa Manyara
imewafikisha katika Mahakama ya wilaya ya Babati, Eva Joseph Mtandika na
Jackline Leonard Manjira kujibu mashtaka ya kuomba na kupokea hongo ya shilingi Milioni moja (TSh.1,000,000/=) kutoka
kwa mfanyabiashara mjini Babati.
Watuhumiwa hao wamefikishwa mahakamani hapo kwa mara ya kwanza leo Juni 15 katika mahakama
ya wilaya hiyo kwa makosa mawili ya kuomba
na kupokea Rushwa kutoka kwa mfanyabiashara mjini Babati.
Katika shtaka hilo la jinai Namba 108 ya mwaka 2020, Upande wa mashtaka
ukiongozwa na mwendesha mashtaka wa TAKUKURU Martin Makani, ulidai mbele ya mahakama kuwa washtakiwa hao kwa
kushirikiana walipokea hongo hiyo toka kwa mfanyabiashara huyo kati ya Juni 6
na Juni 11,2020 mjini Babati ili
wasimpige faini kwa kutotumia mashine ya EFDs na kumtuhumu kuwa hatoi risiti
kwa wateja.
Mwendesha mashtaka Makani alisema washtakiwa hao walitenda makosa hayo kinyume na kifungu cha 15 (1) (a) na kifungu cha 15
(2) cha sheria ya kuzuia na kupambana na rushwa ya mwaka 2007 namba 11.
Hata hivyo washtakiwa wote wamekana mashtaka hayo yanayowakabili ya
kuomba na kupokea hongo ya shilingi Milioni Moja.
Hakimu Victor Kimario aliwataka Washtakiwa hao kila mmoja awe na mdhamini mmoja ambaye atasaini hati ya dhamana ya
shilingi Milioni mbili kila mdhamini ambao wote walikidhi vigezo hivyo na w kwa
dhamana.
Kesi inayowakabili
watumishi hao imeahirishwa hadi Julai 16 mwaka huu itakapotajwa tena kwa
ajili ya kusikilizwa.
Post A Comment: