Basi lililopata ajali maeneo ya kilimatebo wilaya ya Karatu na kusababisha vifo vya watu 3 na majeruhi 25.
Kaimu kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha ACP.Ramadhani Kingai
Kaimu kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha ACP.Ramadhani Kingai
Wito umetolewa kwa medereva kuwa makini na kuchukua tahadhari ya usalama barabarani pindi wanapotumia vyombo vya moto ili kuepusha madhara makubwa ambayo yanaweza kutokea,kwani jeshi la polisi litaendelea kuwachukulia hatua kali za kisheria wale wote ambao wataenda kinyume na taratibu za usalama barabarani
Akitoa taarifa ya ajali kwa waandishi wa habari Kaimu kamanda mkoa wa Arusha ACP.Ramadhani Kingai alisema ajali hiyo ilitokea jana majira ya saa 16:30hrs ,huko maeneo ya Kilimatembo kata ya Rhotia, tarafa ya Mbulumbulu wilaya ya Karatu ,ambapo basi la abiria lenye namba za usajili T.405 AME aina ya Scania mali ya kampuni ya Coastline,lililokuwa linaendeshwa na dereva asiyefahamika kwa majina,liliacha njia na kupinduka baada ya kugongangema upande wa kulia wa barabara,na kupelekea vifo vya watu 3 na majeruhi 25.
ACP Kingai amewataja bado( majina yao hayajafahamika)waliofariki katika ajali hiyo ni mwanamake mwenye umri kati ya miaka 40-45 mwanaume mwenye umeri kati ya mika 30-40 na mtoto mwenye umri wa miezi 6 na walifariki dunia wakipatiwa matibabau katika hospitali ya KKKT Karatu
Majeruhi 7 waliruhusiwa baada ya kupata matibabua,wengine 18 ambao wanaume wapo 8 na wanawake 10 wamelazwa katika hospitali ya kkkt karatu kwaajili ya matibabau zaidi,( 4)kati yao hali zao ni mbaya na taratibu za kuwahamishia katika hospitali ya rufaa mauntmerU Arusha zinaendelea
Alisema chanzo cha ajali hiyo kimesemekana nai uzembe wa dereva kutokuchukua tahadhari za kutosha katika mteremko huo mkali,ambapo mara baada ya ajali kutokea dereva wa basi hilo alitoroka na juhudi za kumtafuta zinaendelea ili hatua zaidi za kisheria zichukuliwe dhidi yake.
Aidha kwa upande wa wasafiri wakiona mienendo ambayo siyo mizuri kwa madereva watoe taarifa kwa jeshi la polisi ili tuweze kuchukuua hatua kabla ya ajali kutokea .
Post A Comment: