Mjumbe wa Bodi ya Nishati Vijijini (REA) Henry Mwimbe (kushoto) akipitia nyaraka baada ya kukagua mradi wa usambazaji umeme REA II unaoendelea katika wilaya za Iramba, Mkalama, Ikungi na Singida DC. Kulia ni Kaimu Mkurugenzi wa Sera na Mipango wa REA, Mhandisi Elineema Mkumbo.
Mhandisi Julius Saady kutoka Kampuni ya Kateth Desco Dynamic Engineering Project Cordinator inayotekeleza mradi huo, akizungumzia hatua waliyofikia ya ujenzi wa mradi huo.
Meneja wa Shirika la Umeme Nchini (TANESCO) Mkoa wa Singida, Abdurahaman Nyenye, akizungumzia maendeleo ya mradi huo. |
Mashimo ya nguzo yakichimbwa.
Upitiaji wa nyaraka za mradi huo ukifanyika.
Na Ismaily Luhamba, Singida.
MENEJA wa Shirika la Umeme Nchini (TANESCO) Mkoa wa Singida, Abdurahaman Nyenye amewaomba wananchi wa vijiji ambavyo bado havijafikiwa na Mradi wa usambazaji Umeme Vijijini (REA) awamu ya pili kujitokeza kwa wingi ili waweze kujipatia huduma hiyo.
Nyenye alitoa ombi hilo kwenye kikao kilichowakutanisha wajumbe wa bodi ya Nishati vijijini Rea pamoja na mkandarasi anayetekeleza Mradi huo.
Alisema kuwa mradi huo ukikamilka, wananchi wajue wazi kuwa gharama za kupata huduma ya umeme zitaongezeka kwani utakuwa chini ya Tanesco ambapo haitakuwa sh.27,000 kama ilivyo hivi sasa.
Mhandisi Nyenye alisema, katika awamu ya pili kulikuwa na vijiji 60 vilivyokuwa havijapata huduma hiyo ambapo mpaka sasa tayari vijiji 24 vimeshafikiwa wakati vijiji 34 na kufanya idadi ya vijiji bado havijafikiwa navyo vipo katika Wilaya ya Mkalama, Iramba, Ikungi na Halmashauri ya Wilaya ya Singida.
Mjumbe wa Bodi hiyo, Henry Mwimbe alitoa wito kwa Wakandarasi wote wanaotekeleza Mradi huo hapa nchini, kuhakikisha wanamaliza kazi hizo kwa wakati ambapo mkataba wao unaisha mwezi Oktoba mwaka huu.
Aidha alisema kuwa kwa sasa mkandarasi anayetekeleza mradi huo mkoani hapa amefanya kazi hiyo kwa asilimia 75 ; hivyo ni matarajio yao kuwa ifikapo mwisho wa mkataba atakuwa amemaliza kazi.
"Mkandarasi ambaye hatamaliza kwa wakati bodi itamchukulia hatua za kisheria." alisema Mwimbe.
Hata hivyo Mkandarasi anayetekeleza mradi huo mkoani hapa, Mhandisi Julius Saady kutoka Kampuni ya Kateth Desco Dynamic Engineering Project Cordinator aliihakikishia bodi hiyo kuwa atamaliza kzi hiyo kwa wakati.
"Kipindi cha nyuma kulikuwa na changamoto ya vifaa, lakini kwa sasa wameshatatua changamoto hiyo hivyo nina uhakika wa kumaliza kwa wakati Mradi huu" alifafanua mkandarasi huyo.
Katika hatua nyingine, Kaimu Mkurugenzi wa Sera na Mipango wa REA, Mhandisi Elineema Mkumbo alieleza mipango ya Serikali ya awamu ya Tano kuwa katika mradi huo, ambao ni REA III awamu ya pili mzunguko wa kwanza, unatekelezwa katika mikoa yote hapa nchini lengo lilikuwa ni kupeleka umeme katika vijiji vyote vilivyo baki.
"Mpaka sasa tumetangaza tenda kwa ajili ya kupata Mzabuni ambaye atatekeleza mradi huu unaotarajiwa kukamilika Juni 30 mwakani ili kutimiza azma ya Serikali hii ya kukipatia huduma ya umeme kila kijiji" alisema Mkumbo.
Post A Comment: