Ikiwa siku ya Jumatatu ya Juni 29,2020 shule zote nchini zikitarajiwa kufunguliwa baada ya maambukizi ya COVID -19 kupungua , Wananchi wa kata ya Chamkoroma wilayani kongwa mkoani Dodoma, wamejitokeza kwa wingi katika ujenzi wa madarasa shule ya sekondari katika kijiji cha Chamkoroma ili kupunguza mrundikano wa wanafunzi madarasani na kutembea kwa umbali mrefu.
Hali hiyo imetokana na wananchi hao kujitolea kuanzisha ujenzi wa madarasa ambayo yatapunguza adha iliyopo katika shule ya sekondari yao.
Awali wakiwa katika ujenzi wa madarasa hayo, Afisa Elimu kata Mwl. Sifrasi J Nyakupora amesema lengo la kuanzishwa shule hiyo ni kutokana na kata hiyo kuwa na ukubwa ikiwa na vijiji saba ambapo wanafunzi hutembea umbali zaidi ya kilomita saba.
Kwa upande wao wananchi wa kijiji cha chamkoroma, Bi. Mwajuma Mwiyoha na mwenyekiti wa kijiji hicho ndugu Nathan Chalo wamesema kutokana na changamoto iiyokuwa ikiwakabili wanafunzi kwa kutembea umbali mrefu kwenda shuleni ndipo walipo amua kuanzisha ujenzi wa madarasa mapya
Akizungumza na wananchi wa kata ya chamkoroma katika ujenzi wa madarasa hayo mkuu wa wilaya ya kongwa, Deogratus Ndejembi akatoa neno kwa wazazi kuwa makini kuwaangalia watoto wao .
Ndejembi amekemea suala la uharibifu wa mazingira na watu kufanya shughuli za kibinadamu katika vyanzo vya maji katika kata hiyo ya Chamkoroma na maelekezo kwa wakala wa misitu TFS wilayani hapo
Post A Comment: