Wakili wa familia ya George Floyd, ambaye kifo chake kiliibua maandamano ya hasira kote nchini Marekani , amemshutumu afisa wa polisi kwa "kupanga mauaji".

Polisi wa Minneapolis Derek Chauvin ameshitakiwa kwa mauaji , lakini wakili Benjamin Crump amekiambia kituo cha habari cha CBS news kuwa yalikuwa ni mauaji ya kiwango cha kwanza.

"Tunadhani kwamba alikua na nia … takriban dakika tisa aliendelea kushindilia goti lake kwenye shingo ya mwanaume ambaye alikua anamuomba amsamehe na kumwambia kuwa hawezi kupumua," alisema

matukio ya uporaji yameripotiwa katika jimbo la Philadelphia.

Video kutoka katika vituo viwili vya televisheni vya Philadelphia Jumapili zilionesha vijana wakivunja magari kadhaa ya polisi na kuiba katika duka moja .


Rais Donald Trump alituma ujumbe wake wa twitter uliosema: Sheria na amri vifuatwe Philadelphia, SASA! Wanapora maduka. Walete wanajeshi wetu waingilie kati ".

Tukio la Floyd limeibua ghadhabu miongoni mwa Wamarekani juu ya mauaji yanayotekelezwa na polisi dhidi ya watu weusi.

Hii inafuatia kesi maarufu ya mauaji ya Michael Brown mjini Ferguson, Eric Garner mjini New York na kesi nyingine zilizowasilishwa mahakamani na vuguvugu linalojulikana kama Black Lives Matters.

Share To:

Post A Comment: