Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Hamisi Kigwangalla akizungumza na Wadau wa Sekta ya Utalii na Waandishi wa Habari leo jijini Arusha wakati wa Uzinduzi rasmi wa Mwongozo wa Taifa wa Uendeshaji wa shughuli za Utalii nchini Tanzania wakati huu wa janga la CORONA.
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Hamisi Kigwangalla (Kulia) na Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii Prof. Adolf Mkenda wakiangalia kurasa na maudhui ya Mwongozo wa Taifa wa Uendeshaji wa shughuli za Utalii nchini Tanzania wakati huu wa janga la CORONA baada ya kuuzindua rasmi leo jijini Arusha.
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Hamisi Kigwangalla akizungumza na Watendaji wa Wizara ya Maliasili na Utalii na Wakuu wa Taasisi zilizo chini ya Wizara ya Maliasili na Utalii leo jijini Arusha mara baada ya Uzinduzi rasmi wa Mwongozo wa Taifa wa Uendeshaji wa shughuli za Utalii nchini Tanzania wakati huu wa janga la CORONA.
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Hamisi Kigwangalla (Katikati), Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Constantine Kanyasu (wan ne kutoka kulia), Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Prof. Adolf Mkenda (wa Pili kushoto) na Naibu Katibu Mkuu Dkt. Aloyce Nzuki, Mkurugenzi Mwendeshaji wa Bodi ya Utalii Tanzania (TTB), Devotha Mdachi na Viongozi wa Vyama vya Mawakala wa Utoaji wa huduma za Utalii nchini Tanzania wakionesha Mwongozo wa Taifa wa Uendeshaji wa shughuli za Utalii nchini Tanzania wakati huu wa janga la CORONA mara baada ya kuzinduliwa rasmi leo jijini Arusha.
Wadau wa Sekta ya Utalii wakifuatilia tukio la Uzinduzi wa Mwongozo wa Taifa wa Uendeshaji wa shughuli za Utalii nchini Tanzania wakati huu wa janga la CORONA.PICHA/Aron Msigwa – WMU
Post A Comment: