Chama cha Mapinduzi (CCM) leo June 12 kimetangaza ratiba ya kuanza kwa mchakato wa kupata wagombea wa nafasi mbalimbali katika chama hiko.
Akizungumza na waandishi wa habari, Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Humphrey Polepole amesema kuwa kanuni wanazo tumia kupata wagombe katika chama hiko inaonesha wazi kuwa hakuna kama CCM huku akiwataka wagombea wawe wanyenyekevu na nidhamu ya hali ya juu wakati wa mchakato ukiwa unaendelea.
"Siku ya leo tunawaanzishia mchakato wa uchaguzi ndani ya CCM, wagombea wa CCM wawe wanyeyekevu sana, kiwango chao cha nidhamu kiwe juu muda wote, wajishushe wasijipeleke mbele, chama kitaketi na kuamua huyu ni bora na anafaa."
''Ratiba ya kumpata mgombea nafasi ya Rais inaanza Juni 15-30, 2020 ambapo itakuwa nafasi ya kuchukua fomu, kutafuta wadhamini na kurejesha,"
"Kiukweli kanuni zetu za kupata wagombea ndani ya Chama kuanzia diwani mpaka rais ni wazi zinaonesha hakuna kama CCM" alisema Polepole.
Post A Comment: