Mbunge wa Jimbo la Dodoma Mjini Mh Anthony Mavunde amegawa vifaa mbalimbali vya kujikinga na maambukizi ya ugonjwa wa COVID 19
kwa Shule zote za Sekondari za umma na binafsi zenye kidato cha Sita.
Mavunde amekabidhi vifaa hivyo vyenye thamani ya zaidi ya Tsh 2,000,000 kwa wakuu wa Shule za Sekondari katika eneo la Jiji ya Dodoma ikiwa ni siku ya kwanza kwa wanafunzi wa kidato cha sita kurejea tena shuleni baada ya agizo la Mh Rais Dr John Pombe Magufuli kuhusu kufunguliwa tena kwa Vyuo na Shule.

"Baada ya Shule kufunguliwa tena nimeona kama Mbunge niunge mkono agizo la Mh Rais kwa kuhakikisha kwamba wanafunzi katika Jimbo langu wanasoma katika mazingira salama na ndio maana nimetoa majaba yenye uwezo wa kuhifadhi lita 1760,Sabuni lita 500,ndoo 50,sabuni boksi 25,Vitakasa mikono 500 na ndoo 50.
Rai yangu ni kuwataka wanafunzi wote wa kidato cha Sita kutumia muda huu kikamilifu kwa kusoma kwa bidii ili kufanya vizuri katika mitihani yenu ya mwisho ili kuendelea kulipaisha Jiji la Dodoma kwenye sekta ya Elimu"Alisema Mavunde
Akishukuru kwa niaba ya Wakuu wa Shule wa Sekondari,Mwl. Aloe Lyimo amemshukuru Mbunge Mavunde kwa msaada mkubwa uliokuja kwa wakati muafaka na kuahidi kutumia vifaa hivyo kwa malengo yaliyokusudiwa.
Post A Comment: