NA HERI SHAABAN
HALMASHAURI ya Ilala Dar es Salaam, imepata hati safi kwa kupindi cha miaka minne mfurulizo kuanzia mwaka 2015/2016 mpaka mwaka 2018/2019.
Akizungumza katika Baraza la Madiwani halmashauri ya Ilala leo Mkaguzi Mkuu wa Nje Manispaa ya Ilala Kutoka Ofisi ya Mdhibiti na Mkaguzi na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali Alestidia Ngalaba alisema manispaa hiyo imekuwa ikifanya vizuri miaka ndani ya miaka minne mfurulizo kuanzia mwaka 2015 /2016 mpaka mwaka 2018 /2019
Ngalaba alisema kwa mujibu wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mwaka 1977 Sheria ya Ukaguzi wa umma ni jukumu la mdhibiti na Mkaguzi mkuu wa Hesabu za serikali kufanya ukaguzi wa taarifa za mapato na matumizi ya fedha za Umma serikali kuu ,Serikali za Mitaa ,Idara na Mashirika ya umma ambapo baada ya ukaguzi, mkaguzi anatakiwa kutoa matokeo ya ukaguzi na mapendekezo kutokana na ukaguzi huo.
" Hati ya ukaguzi kwa mwaka wa fedha 2018/2019 uliokaguliwa, halmashauri ya Ilala imepata hati safi na kufanya halmashauri yetu kuendelea kupata hati safi kwa miaka minne mfurulizo"alisema Ngalaba.
Kwa upande wake Katibu Tawala Wilaya ya Ilala Charangwa Selemani aliwapongeza halmashauri ya Ilala kwa kufanya vizuri kwa miaka minne mfurulizo.
Katibu Tawala Charangwa aliwataka halmashauri ya Ilala kufanya kazi kwa bidii kumsaidia Rais John Magufuli katika usimamiaji wa miradi ya maendeleo.
Naye Katibu Tawala wa Mkoa wa Dar es Salaam Bakati Kunenge alisema wanalizika na utendaji wa Halmashauri ya Ilala wanafanya vizuri zaidi na Wataalam wao.
Katibu Tawala Mkoa aliwataka wafanye kazi kama timu moja katika kipindi cha Rais John Magufuli waongeze vyanzo vingine vya ukusanyaji mapato Menejimenti inafanya vizuri.
Ameagiza halmashuri hiyo kumaliza kwa wakati miradi mkakati ya Rais John Magufuli ambayo ipo halmashauri hiyo ikiwemo machinjio ya Vingunguti na Soko la kisasa la Kisutu ambayo yote ni senemu ya utekelezaji wa Ilani ya Chama cha Mapinduzi CCM.
Aidha alisema manispaa ya Ilala itapanda juu na kuendelea kutumikia wananchi aliwataka wafanye kazi kwa kujiamini ili kuletea heshima mkoa Dar es Salaam na kukiwa na changamoto zozote wafikishe mkoani .
Meya wa manispaa hiyo Omary Kumbilamoto aliwataka Watendaji wa manispaa hiyo kufanya kazi kwa bidii na kusimamia miradi ya maendeleo.
Juni 02/2020
Manispaa ya Ilala
Post A Comment: