Mfanyabiashara Mussa Mohamed akiingia katika mahaka ya hakimu Mkazi jijini Dar es Salaam leo.
MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu imemfutia mashtaka Mfanyabiashara Mussa Mohamed aliyefikishwa mahakamani hapo leo Juni 23, 2020 akikabiliwa na mashtaka ya kusafirisha dawa za kulevya aina ya Heroine.
Hatua hiyo imekuja baada ya Wakili wa Serikali, Sylvia Mitanto kudai mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Yusto Ruboroga kuwa upande wa mashtaka hauna nia ya kuendelea kumshitaki Mohamed kwa kosa hilo.
Aliomba mahakama kufuta shauri hilo chini ya kifungu cha 91(1) cha Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai.
Mapema akisoma mashitaka dhidi ya mshtakiwa huyo, Mitanto alidai mshitakiwa alitenda kosa hilo Juni 5, mwaka huu maeneo ya kuhifadhi mizigo ya wasafiri jijini Dar es Salaam.
Alidai mshitakiwa alikutwa akisafirishwa dawa za kulevya aina ya heroine zenye gramu 101.71.
Hata hivyo mshitakiwa alikana mashitaka na upande wa mashitaka ulidai upelelezi wa shauri hilo bado haujakamilika na kisha wakawasilisha ombi la kumfutia mashtaka.
Hakimu Ruboroga alikubaliana na maombi ya upande wa mashitaka na kuondoa shauri hilo pamoja na kumuachia huru mshitakiwa.
Hata hivyo, mshitakiwa huyo amekamatwa tena na kupelekwa mahabusu ya mahakamani hapo
Post A Comment: