Na Mwandishi wetu, Babati
ALIYEKUWA mjumbe wa mkutano mkuu wa CCM Taifa wa Mjini Babati Mkoani Manyara, Cosmas Bura Masauda amesema Rais John Magufuli alichelewa kuwa Rais wa Tanzania kwani amerudisha nchi kwenye misingi iliyoachwa na Baba wa Taifa hayati Mwalimu Julius Nyerere. 

Masauda akizungumza jana mjini Babati alisema Rais Magufuli ameirudisha Tanzania katika misingi bora hasa CCM kwani hata usipokuwa na fedha unaweza kugombea uongozi. 

Alisema kutokana na Rais Magufuli kuirudisha Tanzania katika misingi ya awali hata watoto wa hayati Nyerere akiwemo Madaraka Nyerere wametangaza kugombea nafasi za ubunge. 

Alisema mwaka 2015 fomu za kugombea ubunge ndani ya CCM ilikuwa shilingi milioni 2.1 na hivi sasa ni sh100,000 ni ishara tosha kuonyesha kililenga matajiri.

"Tofauti na zamani ndani ya CCM kama huna fedha huwezi kuchaguliwa kwa nafasi yoyote na ukisema ukweli utaambiwa huyu ni msaliti au siyo mwenzetu," alisema Masauda. 

Alisema chini ya uenyekiti wa Rais Magufuli na Katibu Mkuu Dk Bashiru Ally CCM imekuwa mpya na ya kimbilio la watu wanyonge tofauti na awali. 

Alisema miaka iliyopita katika eneo lao wagombea waliokuwa na fedha za kuwahonga viongozi wa CCM wa mkoa au wilaya waliitwa waimba kwaya au wanangonjera. 

"Wananchi wa Babati walichukizwa na vitendo hivyo ndiyo sababu wakachagua mbunge na madiwani wa upinzani ila Rais Magufuli alipata kura za urais kwa asilimia 59," alisema Masauda. 

Alisema hivi sasa mjini Babati watia nia ya kugombea ubunge ndani ya CCM wapo zaidi ya 20 wakiwemo walimu 12 na madaktari sita hivyo kuingia ndani kinyang'anyiro cha kuchaguliwa. 

Alisema alisikia baadhi ya viongozi walioangushwa na upinzani wanapitapita mtaani na kudai kuwa kumaliza rushwa ni hadithi ndani ya CCM hivyo viongozi wafuatilie hilo. 

Alisema kutokana na uongozi wa Rais Magufuli hivi sasa hakuna kuibiwa madini ya Tanzanite na wanyamapori kupelekwa nje wala mnyonge kuonewa. 

"Kitendo cha Rais Magufuli kuwateua wapinzani Profesa Kitila Mkumbi, Anna Mghwira na David Kafulila ni uzalendo tosha kwani amewajali hata watoto wa kambo wenye akili hivyo tumuunge mkono," alisema
Share To:

Post A Comment: