Sehemu ya vifaa vya Tehama vilivyotolewa na Mbunge wa viti maalum mkoa wa Arusha Catherine Maggige kwa shule Tatu za sekondari za Makiba Nanja na Ngaranaibo zilizopo kwenye wilaya za Arumeru Monduli na Longido mkoani Arusha vifaa hivyo vyenye thamani ya milion 38 ikiwa ni kuboresha elimu ya tehama na kuongeza Ufaulu kwa wanafunzi wa mkoa huo katika hafla iliyofanyika katika ukumbi wa mkuu wa mkoa wa Arusha leo jijini Arusha picha zote na Ahmed Mahmoud Arusha.

Baadhi ya waalimu wa shule za Makiba Ngaranaibo na Nanja wakifuatilia hafla hiyo ya makabidhiano kwenye ukumbi wa Ofisi ya mkuu wa mkoa wa Arusha leo jijini hapa

Waalimu wakuu wa shule za sekondari wakifuatilia hafla ya kupokea vifaa vya Tehama kutoka kwa Mgeni Rasmi Kaimu KaTawala mkoa wa Arusha David Lyamongi hayupo pichani Leo jijini Arusha katika Ukumbi wa Mkuu wa Mkoa wa Arusha

Afisa Elimu Taaluma mkoa wa Arusha Joseph Ngoseki akiongea kwenye Hafla ya kukabidhi vifaa vya Tehama kwa shule tatu zaSekondari za mkoa wa Arusha zilizopo kwenye wilaya Tatu za Monduli,Longido na Meru jijini Arusha



Na Ahmed Mahmoud Arusha
Mbunge wa viti maalum mkoa wa Arusha Catherine Maggige Amezitaka shule mkoani Arusha
kuhakikisha wanaongeza ufaulu kwa wanafunzi ikiwemo masomo ya tehama
kwa kuwa dunia inaelekea kwenye teknolojia hiyo ya mawasiliano kwa
sasa.
Maggige ameyasema hayo kwenye hafla ya kukabidhi vifaa vya tehama
zikiwemo Kompyuta 25 na mashine za kudurufu vyenye thamani ya milion
38 aliyowakilishwa na mratibu wake Philip Amoh kwa shule tatu za
Ngarnaibo Makiba na Nanja zilizopo kwenye wilaya za Arumeru,Monduli na
Longido mkoani Arusha
Alisema kuwa Msingi huo utasaidia sana kuongea uelewa wa elimu mtandao
na kuwasaidia vijana wa mkoa wa Arusha kuongeza maarifa zaidi
yatakayosaidia kwenda na teknolojia hiyo ya mawasiliano.
"Wakuu wa shule na maafisa elimu hakikisheni mnavisimamia vyema vifaa
hivi kwa lengo la kuongeza wigo mpana wa ufaulu kwa vijana wetu na
tukiona matumizi yameenda kama malengo yalivyo kusudiwa tutaweza
kuongeza nawashukuru sana mfuko wa fursa sawa kwa wote kwa
kushirikiana nami kutoa msaada huu wenye thamani ya milion 32"
Kwa Upande Kaimu Katibu tawala wa mkoa wa Arusha David Lyamongi
alisema kuwa vifaa hivyo mashine za vidurufu na kompyuta vitasaidia
kuboresha elimu ya teknolojia ya mawasiliano kwa shule zetu na
kuwataka wote waliopewa kwenda kuvitumia kwa malengo yaliokusudiwa.
Alisema kuwa ongezeko la vifaa hivyo kwa shule zetu mkoani Arusha kwa
ujumla vimesaidia kuongeza ufaulu kwa wanafunzi hivyo kuendelea
kumpongeza mbunge huyo kwa kuendelea kushirikiana na serikali ya mkoa
kukuza elimu kwa vijana wetu mashuleni.
"Naomba nitumie fursa hii kumpongeza mbunge Catherine kwa kuwa amekuwa
mstari wa mbele na msaada kwetu kwa muda mrefu ametutetea na kusaidia
serikali kwenye shughuli mbalimbali za kijamii katika mkoa naomba

Share To:

Arusha Newsroom

Post A Comment: