Katika ziara ya ukaguzi wa ujenzi wa jengo la Ofisi Umoja wa posta barani Afrika PAPU wa kwanza kushoto ni Katibu mkuu wa umoja huo Younnus Djibrine akipata baadhi ya maelezo kuhusu maendeleo ya ujenzi wa mradi huo unaoendelea jijini Arusha .
Baadhi ya wakazi wa Arusha walio pata fursa za ajira katika mradi wa ujenzi wa jengo la makao makuu ya Umoja wa Posta afrika wakiwa katika shughuli za ujenzi katika hatua za awali kuhusu ujenzi wa jengo hilo la kisasa linalo tajwa kugharimu zaidi ya bilioni 38 huku asilimia 40 zikiwa kutoka serikali ya Tanzanaia
Msimamizi Mkuu wa mradi Mhandisi Hanington Kagiraki wa kwanza kulia akifafanua baadhi ya Mambo kuhusu mradi wa ujenzi wa jengo la makao makuu ya Umoja wa Post Afrika PAPU wapili kulia ni katibu mkuu Wizara ya Ujenzi Uchukuzi na mawasiliano Tanzania Dkt Zainabu Chaula.
Na:Vero Ignatus-Arusha.
Zaidi ya shilingi bilioni 38 zimetengwa kwa ajili ya ujenzi wa jengo la kisasa lenye jumla ya ghorofa 17 ambalo linajengwa kwa ubia Kati ya Umoja wa Post Afrika (PAPU) na serikali ya Tanzania kupitia Mamlaka ya mawasiliano Nchini (TCRA).
Ni miezi sita sasa tangu kuzinduliwa shughuki za ujenzi kwa kuwekewa jiwe la msingi na Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na mawasiliano mnamo januari 18 mwaka 2020 zoezi lililo ongozwa Mhandisi Isack Kamwelwe alie ambatana na viongozi mbalimbali Nchini na Nchini wanachama wa umoja huo barani Afrika.
Katika zoezi la ukaguzi wa maendeleo ya ujenzi huo Serikali kupitia Wizara ya Ujenzi ikiongozwa na katibu mkuu wa Wizara hiyo Dkt Zainabu Chaula alie ambatana na baadhi ya viongozi akiwemo Katibu mkuu wa umoja wa posta afrika Younnus Djibrine wametembelea eneo Hilo ya ujenzi na kuoneshwa kuridhishwa na Hatua za awali za ujenzi.
"Malengo ya ziara yangu ni kukagua maendeleo ya ujenzi wa jengo la ofisi za PAPU litakalo kuwa na ghorofa kumi na Saba,jengo hili litakapo kamiliaka litakuwa na Ofisi za makao makuu ya Umoja huu na litatumika kwa shughuli mbalimbali zikiwemo benki,maduka,migahawa,posta na maeneo ya kupangisha kwa matumizi mbalimbali kibiashara"Alisema Dkt Zainabu.
Amesema jengo Hilo la kisasa litajumuisha nafasi maalumu kwa ajili ya shughuli za kitalii,na wananchi ili kujionea vivutio mbalimbali ikiwemo mlima wa Kilimanjaro unaopatika Nchini Tanzania.
Serikali imebainisha kuwa kwa kipindi cha miezi sita tangu ujenzi kuanza,kazi ya ujenzi imeendelea vyema kwa kuzingatia tahadhari kwa Wafanyakazi,pamoja na viwango vya ubora.
"Tangu kuanza kwa ujenzi hapa wazawa wamekuwa wakipewa nafasi ya kwanza ambapo asilimia kubwa ya wananchi hususani vijana wameweza kupata fursa za ajira ili kuweza kujiongezea kipato kwa maslahi ya familia zao,kwa kuzingatia masimamizi Mkuu wa ujenzi ni Mhandisi mzawa wengi wao wamepata ajira za moja kwa moja"alisema Katibu mkuu Wizara ya Ujenzi.
Kwa upande wake katibu mkuu wa umoja wa posta afrika Younnus Djibrine amesema yeye Kama Mtendaji kwa namna moja ama nyingine amekuwa akifanya ukaguzi wa ujenzi kwa kutembelea eneo hilo ili kujionea shughuli zinavyo endelea kwa maslahi ya Umoja wa nchi wanachama wa posta barani Afrika.
"Ujenzi huu Ni sehemu ya matunda ya Umoja wa PAPU na ndio maana hata viongozi wetu wa nchi mfano Rais Magufuli amekuwa akihimiza kuchapa kazi naamini matunda haya ni kwa faida yetu site"
Michuzi blog imezungumza na baadhi ya vijana walio pata fursa ya ajira katika ujenzi huo akiwemo Stanel Kilango na Julius Lena wanasema kwa Sasa maisha yao yamebadilika kutoka na nafasi walizo pata katika utekelezaji wa mradi huo wa ujenzi Nchini Tanzania.
"Maisha yangu kwasasa yana unafuu mno maana awali nilikuwa nimejiajiri mwenyewe katika shughuli zangu binafsi ukiwemo biashara ndogondogo dah kwa Sasa nashukuru mungu Mambo yameanza kubadilika naomba serikali ya Tanzania iendelee kuleta miradi mikubwa namna hii kwa maslahi ya wazawa"alisema Stanel.
Baadhi ya wanafunzi kutoka vyuo vya ufundi Nchini wamekuwa wakitumia fursa ya ujenzi wa jengo Hilo la kisasa kujifunza kwa vitendo ili kuweza kujijengea uzoefu wa kazi baada ya kuhitimu mafunzo yao.
Post A Comment: