MWENYEKITI wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi Taifa (UVCCM), Heri James ametangaza kuwa jumuiya hiyo inawarejesha kazini wajumbe sita wa umoja huo Zanzibar waliokuwa wakituhumiwa kutoa na kupokea rushwa.
Akizungumza jijini Dodoma na waandishi wa habari, Heri amesema kwamba uamuzi huo ni baada ya uchunguzi uliokuwa ukifanywa na Mamlaka ya Kuzuia Rushwa na Uhujumu Uchumi Zanzibar (ZAECA) kukamilika na kukutwa hawana hatia.
Amewataja wajumbe hao kuwa ni Pandu Salum Sungura, Mwenyekiti wa UVCCM Mkoa wa Kaskazini Unguja, Amina Bakari Yusuph Mjumbe wa Baraza Kuu la UVCCM Mkoa wa Kaskazini Unguja, Alawi Hadali Faumu Katibu wa UCCM Mkoa wa Kaskazini Unguja, Fransisca Clement Mjumbe Baraza Kuu la UVCCM Mkoa wa Mjini Hussein Ayub Idd ,Mjumbe Baraza Kuu la UVCCM Mkoa wa Mjini Lulu Mwacha Mjumbe Baraza Kuu la UVCCM Mkoa wa Arusha.
“Tulifanya uamuzi wa kuwasimamisha wajumbe hawa kupitia kamati ya utekelezaji kutokana na tuhuma zilizoibuliwa za kutoa na kupokea rushwa. Leo ninavyozungumza taasisi ya ZAECA imewasiliasha taarifa rasmi CCM kwamba vijana hawa hawakuhusika, nataka niwaambie vijana wa CCM katika hili hatuna mzaha na yeyote atakayebainika akifanya vitendo hivi tutamchkulia hatua kama watu wengine bila ubaguzi,” amesisitiza James.
Pia ameipongeza ZAECA na Jeshi la Polisi kwa kutimiza majukumu yake kwa weledi bila upendeleo pamoja na kuwapongeza vijana hao kwa utulivu waliokuwa nao wakati wote wa kusimamishwa kwao akiwatka wanaporudi katika majukumu yao kuwa na ari ya kufanya kazi kwa uaminifu kwa manufaa ya chama na taifa kwa ujumla.
Katika hatua nyingine Heri amesema anasikitishwa na taabia ya baadhi ya watu kuwafanyia vitendo vya udhalilishaji na kejeli kwa baadhi ya wagombea waliojitokeza kuchukua fomu za kugombea nafasi mbalimbali kutokana na jinsia zao au kwa sababu aliwahi kushika nafasi katika taasisi za umma akisema kwamba kugombea ni haki ya kila Mtanzania kwa mujibu wa katiba ya nchi.
“Kumekuwa na siasa za kuwashutumu kwasabau tu wamewahi kuwa viongozi wa umma huko Zanzibar na sababu nyingine niseme kugombea ndani ya Chama cha Mapinduzi niwakumbushe Watanzania suala la kugombea haki ya kikatiba kwa kila raia haijalishi aliwahi kuwa nani, wapi na kwa maslahi gani na kugombea kwa chama chetu pia ni haki ila vikao tutavitumia kuchambua nani anafaaa kwa wakati huo,” amekemea Mwenyekiti huyo.
Aidha amewataka vijana wa CCM kujitokeza kwa wingi kugombea nafasi mabalimbali ikiwemo udiwani katika meneo yao akisema kwamba vijana ni jeshi kubwa lenye nguvu hivyo ni wakati wao sasa kuonyesha uwezo wao kwa manufaa ya wananchi na kwamba maendeleo yapo mikononi mwa vijana.
“Sasa hivi tunajiandaa na uchaguzi mkuu na tayari fomu zimeanza kuchukuliwa vijana mna nafasi kubwa sana jitokezini mchukue fomu maana mna uwezo mkubwa hukuna haja ya kuhofia sijui kipato, uwezo wako ndio utakaokubeba na hata ikitokea hujapata nafasi basi shikirikiana na waliopata tuijenge nchi yetu” ameeleza.
Mwenyekiti huyo amehitimisha kwa kuwataka Watanzania kushirikiana kwa pamoja katika kukemea na kupiga vita vitendo vya rushwa mahali popote hasa wakati huu wa uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika mwezi Oktoba mwaka huu.
Post A Comment: