Mkuu wa
Jeshi la Polisi Nchini IGP Sirro amesema kuwa, Nchi Wanachama wa Jumuiya ya
Shirikisho la Wakuu wa Majeshi ya Polisi wa Nchi za Ukanda wa Kusini Mwa Afrika
(SARPCCO) wamekubaliana kwa pamoja kuendelea kupambana na uhalifu ili kutokutoa
mwanya kwawahalifu ndani ya jumuiya hiyo.
IGP Sirro
amesema hayo leo jijini Dar es salaam wakati aliposhiriki mkutano wa Jumuiya
hiyo uliofanyika kwa njia ya mtandao (video conference) mkutano ambao umelenga
kuwekeana mikakati mbalimbaliya kiutendaji ndani ya jumuiya hiyo.
Akizungumzia
suala la uhalifu kwa njia ya mtandao IGP Sirro amesema kuwa, jambo kubwa ambalo
jumuiya hiyo wamekuwa wakipambana naloni kuendelea kufanya mafunzo ya mara kwa
mara hasa kwa wapelelezi ili kuwa na vifaa, uweledi na uelewa juu ya masuala ya
uhalifu wa kimtandao.
Katika hatua
nyingine IGP Sirro ameelezea juu ya ushirikiano kati ya nchi wanachama wa
jumuiya hiyo hasa katika kipindi hiki cha kuelekea kwenye uchaguzi mkuu.
Post A Comment: