Mkuu wa Mkoa wa Singida, Dkt. Rehema Nchimbi akizungumza na wananchi wa Kata ya Msange wakati akikagua Kituo cha  Afya cha kata hiyo juzi.
Wauguzi  wakimsikiliza RC Dkt.Nchimbi.

Wananchi  wakimsikiliza RC DKkt.Nchimbi eneo itakapo jengwa Stendi Njia Panda ya Meliya.
Wananchi  wakimsikiliza RC DKkt.Nchimbi
Wananchi  wakiwa kwenye eneo itakapojengwa Stendi ya Mabasi.





Na Ismail Luhamba Singida


Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt Rehema Nchimbi Ameiagiza Halmashauri ya Wilaya ya Singida kuweka waazi Ramani ya kituo cha mabasi kwa wananchi.

Halmashauri ya Wilaya ya Singida imeagizwa kuweka wazi mapema ramani ya kujenga vibanda katika kituo cha magari ya abiria kinachojengwa ndani ya halmashauri hiyo ili kuondoa usumbufu.

Agizo hilo limetolewa wakati akihitimisha ziara yake ya kutembelea wilaya zote za mkoa wa Singida kwa ajili ya kukagua miradi ya maendeleo.

Dkt. Nchimbi alitembelea kituo hicho kilichopo katika Kijiji cha Kinyamwenda kinachotarajiwa kukamilika mwezi Agosti mwaka huu kwenye mwendelezo wa ziara yake Mkoani humo.

Alisema kuwepo kwa kituo hicho kitatoa ajira kwa vijana akinamama na wananchi wa kijiji hicho pamoja na vijiji jirani na halmashauri kupata mapato.

"Halmashauri hii ya Singida ilijulikana kuwa nyuma sana kiuchumi na kuna watu walikuwa wanatamani kuhama,sasa hawatahama, kwani kuna kituo cha magari ya abiria, kiwanja cha kimataifa cha mchezo wa Olympic na michezo mingine." alisema Nchimbi.

Katika hatua nyingine Dkt. Nchimbi ameahidi kutoa pikipiki mmoja kwenye kituo cha Polisi kata ya Msange baada ya wazee wa Kata hiyo kutoa kwake ombi hilo kutokana na utendaji kazi mzuri wa jeshi hilo.

Akitoa ombi hilo kwa Mkuu wa Mkoa pamoja na kuipongeza Serikali ya Rais Magufuli kwa mambo makubwa iliyofanya kwenye Kata hiyo katibu wa Wazee Kata hiyo, Philemon Mnyawi alisema hawajatumwa na mtu bali kutokana na utendaji kazi mzuri wa vijana hao ndio wakaamua kuwaombea pikipiki hiyo ili iendelee kuwasaidia katika kazi zao.

"Hatujatumwa na mtu wala Polisi hawajatutuma Mkuu wa Mkoa,tumejituma sisi Wazee wa Msange,tunakuomba uwapatie pikipiki moja tu vijana wetu hawa wanafanya kazi nzuri sana."alisema Mzee Mnyawi.

Aidha Dkt Nchimbi alipata fursa ya kutembelea kituo cha afya Msange ambapo Mganga Mkuu wa kituo hicho, Sarah Nkundi alipongeza hatua ya Serikali ya kupeleka vifaa vya kisasa kwenye kituo hicho na kukiita kituo hicho Hospitali kutokana na hadhi yake.

"Zile huduma ambazo wagonjwa walipaswa kuzipata katika Hospitali kubwa zipo hapa,vifaa ambavyo tulizoea kuviona Hospitali kubwa vipo hapa." alisema Nkundi.


Share To:

Post A Comment: