Na Joachim Nyambo,Mbeya.

TANZANIA imeshauriwa kujiandaa kupokea wageni kutoka mataifa mbalimbali duniani watakaokuja kwaajili ya kujionea maajabu mbalimbali yanayoendelea kutokea nchini ikiwemo maamuzi magumu na yenye tija ya Rais John Magufuli.
Miongoni mwa mambo yanayotajwa kuwa kivutio kwa wageni kutoka mataifa ya mbali ni pamoja na maamuzi aliyoyafanya rais Magufuli ya kutowafungia ndani wananchi kutokana na ugonjwa wa Homa kali ya mapafu inayosababishwa na virusi vya Corona maamuzi aliyoyasimamia mpaka maambukizi yanatajwa kupungua kwa kasi nchini.
Ushauri huo ulitolewa na Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Elimisha Tanzania lenye makao yake makuu jijini Mbeya,Festo Sikagonamo alipozungumzia utendaji kazi wa Serikali ya awamu ya tano chini ya rais Magufuli.
Sikagonamo alisema mambo yaliyofanywa na Magufuli ni makubwa na yanamtofautisha na viongozi  wengine Duniani jambo linaloonekana kuzua gumzo katika mataifa mbalimbali yakiwemo makubwa na yenye kupenda kunyenyekewa siku zote.
Alisema sababu hiyo itaifanya Tanzania kupokea wageni wengi zaidi kutoka mataifa mbalimbali duniani ambao watakuja nchini si tu kwa ajili ya kuangalia vivutio vya utalii vilivyopo bali wengine watakuja kuifahamu Tanzania ilivyo sambamba na utawala wake.
“Wengine watakuja wakiwa na shauku kubwa ya kutaka kumwona mubashara Rais Magufuli… kwamba ni mtu wa namna gani…ana fananaje kutokana na mambo mazuri makubwa anayoyafanya kwa ajili ya taifa la Tanzania.”alisema Sikagonamo
“Rais Dkt. John Magufuli ametumia fikra bunifu na za kipekee kwanza kwa kuifanya Corona kama vita na sio janga la kiafya linalohitaji mashauri ya kisayansi.Haya yalikuwa maono ya kitofauti ikifananishwa na viongozi wa mataifa mengine”aliongeza.
Mkurugenzi huyo alimtaja Rais Magufuli kuwa wa kipekee ulimwenguni ambaye alitumia mbinu bunifu na za kipekee kwa namna alivyofanya uchunguzi katika maabara ya kitaifa jambo lililoyasaidia pia mataifa mengine kufikiri mbali ya mitazamo yao ya awali.
“Ni rais Magufuli pekee ambaye hakutaka kuiga au kuingia mkumbo wa nchi nyingine kwa kuwafungia watu ndani bali aliwatoa hofu wananchi na aliwasisitiza kufanya kazi ili kuendeleza uzalishaji.Licha ya mashirika ya kimataifa na nchi kubwa duniani kuitishia Tanzania kuitaka ifungie watu, lakini kamwe Magufuli hakuteteleka.”alisema.
Alisema jambo lililozidi kuwapa moyo watanzania na kuwaondoa shaka waliyokuwa nayo awali baada ya kuona rais wao anakwenda tofauti na viongozi wengine ni pale Magufuli alipousaajabisha ulimwengu kwa kutabili mambo mbalimbali ambayo baadye yalikuja kuigwa na Shirika la Afya Duniani (WHO).
Aliongeza kuwa kutokana na msimamo wake rais Magufuli amepunguza tishio la ugonjwa wa Corona na kuhamasisha utumiaji wa tiba za asilia kama vile kunywa tangawizi na chai ya limao, na tiba ya kufukiza kama njia ya kuzuia kuambukizwa kwa COVID 19.
Aliitaja pia hatua ya Tanzania kupeleka ndege Madaska kuchukua Dawa kwa ajili ya kuifanyia utafiti ili kuweza kusaidia watu wake kuwa ya kijasiri na yenye kulenga misimamo ya kutetea watu wake kwa njia zinazoonekana zinafaa kwa maamuzi ya Taifa husika badala ya kusubiri mataifa yanayojiona ndiyo wasemaji na wenye maamuzi ya mwisho.
Hatua ya Rais magufuli kuwa wa kwanza kufungua safari za anga ili kuruhusu ndege za kimataifa kutua nchini Tanzania aliitaja kuwa yenye kulenga zaidi maslahi ya Taifa kwakuwa kufanya hivyo kunazidi kuwapa moyo wa kufanya kazi kwa kujittuma wananchi kwakuwa Corona huenda ikachukua muda mrefu hivyo kutofanya kazi kutaweza kuleta athari nyingi mbaya na kubwa ndani ya jamii.


Share To:

Post A Comment: