NA HERI SHAABAN


CHAMA CHA Mapinduzi CCM Wilaya ya Ilala kimepokea waliokuwa madiwani sita wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA)TLP na ACT katika kikao cha Halmashauri Kuu Wilaya ya Ilala .

Akipokea madiwani hao Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Ilala Ubaya Chuma alisema katika uchaguzi Mkuu wa Rais Wabunge na madiwani chama hicho kitashinda majimbo pamoja na Kata.

Ubaya Chuma alisema Chama cha Mapinduzi CCM kimejipanga vizuri kuakikisha kinashinda kwa kishindo.

Akizungumzia kuwapokea waliokuwa madiwani wa CHADEMA alisema CCM ni nyumbani wote watarudi.

Wakati huo huo Mwenyekiti Ubaya Chuma aliwataka wana CCM kushirikiana katika kuisaidia halmashauri suala la ukusanyaji wa mapato kuakikisha halmashauri ya Ilala inavuka lengo.

Pia aliwataka  Wenyeviti wa Serikali za Mitaa  wa Halmashauri ya Ilala wafanye kazi kwa weledi kwenda na kasi ya Rais John Magufuli ikiwemo kusimamia miradi ya maendeleo  na kutatua kero za wananchi wa kila eneo.

"Naomba Wenyeviti wa Serikali za mitaa msimamie majukumu yenu msiwe chanzo cha migogoro yenu, Mwenyekiti atakayekwenda kinyume atavuliwa madaraka yake"alisema Chuma

Akiwataja madiwani hao alisema  Kassim Msham, Dorcus Rukiko, Bonaventure Mphuru, Edwin Mwakatobe, Joseph Ngoa, na Joseph Saenda.


Kwa upande wake Katibu wa CCM wilaya Ilala Idd Mkoa aliwataka wana CCM kuchapa kazi kwa bidii kuunga mkono juhudi za Rais katika  kujenga Tanzania ya Uchumi wa viwanda.

Naye aliyekuwa Diwani wa CHADEMA Kata ya Pugu Bonaventure Mphuru alisema Ilani ya CCM inatekelezwa vizuri yupo pamoja na Rais John Magufuli  ,aliwataka Watanzania kumtumia Rais vizuri.


Mwisho
Kikao cha Halmashauri Kuu CCM Wilaya ILALA
Share To:

TANGA RAHA BLOG

Post A Comment: