SERIKALI kupitia Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto imejenga Maabara ya Kisasa ya uchunguzi wa magonjwa ya binadamu ya kuambukiza yenye thamani ya shilingi Bilion tisa katika Wilaya ya Siha Mkoani Kilimanjaro.
Hayo yamesemwa na Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Godwin Mollel alipofanya ziara ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa Maabara hiyo ikiwa inaelekea kukamilika ili kuanza kutoa huduma za uchunguzi wa magonjwa ya kuambukiza.
“Mmekuwa mkisikia mara nyingi nikisema kwamba tunajenga maabara ya kisasa yenye thamani ya shilingi Bilion tisa kwenye Wilaya ya Siha, lakini leo tunaliona jengo hilo lenye thamani hiyo” alisema.
Aliendelea kusema kuwa, tangia Uhuru wa nchi yetu mpaka 2015, Serikali Serikali Serikali ilikuwa na Hospitali za Wilaya sabini na saba tu, huku akiweka wazi kuwa tangia Serikali inayoongozwa na Dkt. John Pombe Magufuli iingie madarakani tayari Hospitali za Wilaya 67 zimekwisha jengwa ili kuboresha upatikanaji wa huduma za Afya.
“Toka Uhuru tumekuwa na Hospitali za Wilaya sabini na saba, lakini kwa miaka hii mitano Hospitali zilizokwisha jengwa ni sitini na saba na kwenye bajeti hii, mpaka 2021 zitaenda kuwa karibia 90, maana yake tukienda kwa kasi hii huduma za Afya zitakuwa nzuri sana” alisema.
Nae Mkuu wa Wilaya ya Siha Mhe. Mhe. Onesmo Buswelu amemshukuru Mhe. Rais Dkt. John Pombe Magufuli kwa kutoa fedha nyingi kwaajili ya ujenzi wa Maabara hiyo ya magonjwa ya kuambukiza ambayo itakuwa msaada mkubwa kwa wananchi wa Siha Kilimanjaro na Tanzania kwa ujumla.
“Tunaishukuru Serikali kwa kutoa fedha nyingi kwa wananchi wa Wilaya ya Siha, lakini kwa Watanzania kwa ujumla kwasababu masuala ya magonjwa ambukizi yanaenda kuchunguzwa na kutibiwa hapa” alisema.
Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Kibong’oto Dkt. Riziki Kisongo amesema kuwa, mradi huu utakuwa na manufaa makubwa kwa Hospitali na nchi kwa ujumla kama kupanua wigo wa kuchunguza vimelea vya magonjwa ambukizi kama vile Corona, pia itatumika kufanya tafiti za changamoto za magonjwa ambukizi nchini na kuelimisha Wataalamu mbali mbali nchini.
“Mradi huu ambao unakaribia kukamilika sio mda mrefu utakuwa na manufaa sana kwa hospitali na kwa nchi nzima, kwanza utapanua wigo wa kuchunguza vimelea vya magonjwa ambukizi hatari kama vile vya Corona na virusi vingine, pia utatumika katika kufanya tafiti mbali mbali za changamoto ya magonjwa ambukizi nchini, na utaweka faida ya kuelimisha Wataalamu mbali mbali katika nyanja ya Maabara ambao watakuwa rasilimali kubwa nchini kwetu ” alisema.
Post A Comment: