NA ANDREW CHALE, ZANZIBAR

WACHUKUA fomu za Urais ndani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) limeendelea tena kwa mchana wa leo kwa  aliyekuwa Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi  (ZEC), Jecha Salum Jecha kuchukua fomu na kufikisha Makada 14 hadi sasa.

Jecha alifika majira ya saa nane na dakika 46 na kisha kupanda moja kwa moja kupokea fomu hiyo ambayo inalipiwa shilingi milioni moja.

Baada ya tukio hilo Jecha alipata wasaha wa  kuzungumza na wanahabari ikiwemo kuulizwa maswali.

Ambapo lengo kuu la kuchukua fomu alieleza kuwa, endapo atapata nafasia kupitishwa na chama chake anataka kuleta usawa na umoja kwa Wazanzibar wote bila kuangalia dini ama rangi zao.

"Dhumuni langu nikipata riadhaa ya kugombea ni kutaka kuwaunganisha wananchi wote wa Zanzibar na Watanzania kwa ujumla.

...Katika shughuli za kimaendelea na shughuli zingine. Nitajitahidi kwa kadri endapo chama changu kitanisaidia.
Nitasaidia kwa haki bila kubagua dini wala rangi." Alieleza Jecha Salum Jecha mbele ya Wanahabari.

Aidha, alieleza kwa kifupi historia yake ikiwemo elimu na uzoefu wake wa kikazi.

Jecha alisema amezaliwa Unguja, Zanzibar mwaka 1952. Elimu ya Msingi alihitimu mwaka 1959, Sekondari mwaka 1966.

Elimu ya Chuo alihitimu Chuo Kikuu cha Mlimani Dar es Salaam (UDSM) mwaka 1977 na kupata Shahada yake ya kwanza.

Shahada yake ya pili aliipata nchini Marekani katika Chuo cha New York.

"Uzoefu wangu mimi nilikuwa Mwalimu. Mwaka 1972 nilianza Serikalini.

Mwaka 1980 niliendelea ndani ya Serikali kuu hadi 1988.
Nliwahi kuwa mjumbe wa tume ya uchaguzi  ZEC, 208. Baada ya hapo Nilikuwa Mwenyekiti hadi 2018 nilipostaafu rasmi." Almalizia Jecha.

Jecha alipata kugonga vichwa vya habari  baada ya uamuzi aliouchukua wa kufuta uchaguzi wa Zanzibar wa mwaka 2015 ambapo aliwahi kunukuliwa kuwa alichukua maamuzi hayo baada ya kubainika kuwa na dosari, ulifanyika kwa kufuata taratibu, kanuni, Sheria na Katiba ya Zanzibar.

Kwa leo anakuwa Kada pekee kujitokeza kuchukua fomu hiyo na kuwa wa  Kada pekee wa kufikisha idadi yao 14.

Wengine ni:

Waziri wa Maji wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzaniaa, Profesa Makame Mbarawa, Mwanamama, Mwatum Mossa Sultan,  Haji Rashid Pandu na Dkt. Abdulhalim Mohammed Ali.

Pia wamo: Shamsi Vuai Nahodha, Mohammed  Jafari Jumanne, Mohammed Hija Mohammed.

Pia wamo Balozi Meja Jenerali Mstaafu, Issa Suleiman Nassor,
Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa,  Dk. Hussein Mwinyi aliyekuwa Mbunge wa jimbo la Kwahani Mjini Unguja, Zanzibar.

Pia Mbwana Bakari Juma, Balozi Ali Karume, Mbwana Yahaya Mwinyi na Omary Sheha Mussa.

Tukio la kukabdhiwa fomu linatarajiwa kufungwa rasmi 30 Juni huku likisimamiwa na Katibu wa Idara ya Organization CCM, Zanzibar, Cassian Galos.

MWISHO.
Share To:

Post A Comment: