Na Editha Karlo, Kigoma
WATU tisa wamefariki baada ya boti la abiria kuzama katika ziwa Tanganyika.
Kamanda wa polisi mkoa wa Kigoma Kamishna msaidizi MARTIN OTTIENO amethibitsha kutokea kwa ajali hiyo katika eneo la rasini na kusema kuwa Boti ilo liitwalo mv Nzeimana linalofanya safari zake kati ya Kijiji cha Sibwesa na ikola limezama likiwa abiria sitini ambapo abiria hamsini na moja wameokolewa.
Aidha Kamanda OTTIENO amesema chanzo cha ajali hiyo ni upepo mkali uliosababisha boti hilo kukosa muelekeo na hatimaye kupinduka.
Post A Comment: